Friday, April 15, 2016

Drogba kushtaki gazeti la daily mail

Nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea Didier Drogba amesema atachukua hatua za kisheria dhidi ya gazeti la Daily Mail. Hii ni baada ya gazeti hilo kuchapisha habari zinazodai kwamba kati ya pesa anazokusanya kupitia wakfu wake wa kusaidia jamii, ni chini ya asilimia moja zinazotumiwa kufaa jamii. Gazeti hilo limesema ni £14,115 pekee kati ya £1.7m zinazotolewa na wachezaji nyota na wafanyabiashara ambazo husaidia watoto Afrika. Drogba, 38, ametoa taarifa akisema habari hizo ni za “uongo na za kumharibia sifa”. Drogba anataka kuwa kocha wa Chelsea Drogba hatarejea Chelsea Tume inayodhibiti mashirika ya kusaidia jamii yaliyosajiliwa Uingereza imesema inachunguza “madai ya ukiukaji wa sheria”. Kwenye taarifa yake, Drogba amesema: “Hakuna ulaghai, hakuna ufisadi na hakuna udanganyifu.” Drogba, raia wa Ivory Coast, anayechezea klabu ya Montreal Impact ya Canada kwa sasa amewatuhumu wanahabari wa Daily Mail kwa kuweka hatarini maisha ya maelfu ya watoto wa Afrika. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako

Rais magufuli amfuta kazi mharir wa magazeti ya serikali

AFP Rais wa Tanzania John Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw Gabriel Nderumaki. Bi Tuma Abdallah, ambaye amekuwa mhariri mtendaji msaidizi wa magazeti ya serikali (TSN), ameteuliwa kuwa kaimu. Hakuna maelezo yoyote zaidi yaliyotolewa kuhusu sababu za kutenguliwa kwa uteuzi wa Bw Nderumaki. TSN huchapisha magazeti ya Daily News, Sunday News, habari Leo, Habari Leo Jumapili na Spoti Leo. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako

Friday, April 8, 2016

Kampuni ilitaka kukwepa kodi uganda

Kampuni ya mafuta ilitaka kukwepa kodi Uganda 7 Aprili 2016 Imebadilishwa mwisho saa 17:17 GMT Ushahidi mpya uliotokana na nyaraka zilizofichuliwa za Panama zimefichua jinisi kampuni ya kuchimba mafuta iliyopo Uingereza iliyo na uhusiano na chama tawala ilivyojaribu kukwepa kulipa dola milioni 400 za kodi kwa serikali ya Uganda. Barua pepe zilizofichuliwa na muungano wa waandishi wapelelezi wa kimataifa ICIJ na zilizosambazwa kwa BBC zinaonyesha kuwa kampuni hiyo ilifahamu kuhusu malipo hayo ya kodi yanayohusu uuzaji wa hisa zake katika biashara ya mafuta Uganda. Mapendekezo yaliwasilishwa baadaye ili kukwepa kulipa deni hilo kwa kuhamisha usajili wa kampuni hiyo kutoka Bahamas hadi Mauritius.

Matandika asimamishwa kazi TFF

Matandika asimamishwa kazi TFF Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine amemsimamisha Juma Matandika kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma zinazohusiana na hadhi za wachezaji, shirikisho hilo limesema.

Maasi ya kikurd 1991

wenzako Mpiga picha Richard Wayman anakumbuka akifanya kazi maeneo ya kaskazini mwa Iraq wakati wa maasi ya Wakurdi mwaka 1991. Baada ya zaidi ya mwezi wa mashambulio ya angani na kipindi kifupi cha mashambulio ya ardhi ya wanajeshi wa muungano ulioongozwa na Marekani dhidi ya wanajeshi wa Saddam Hussein, Vita vya Ghuba vya 1991 vilikaribia kumalizika. Lengo la kukomboa Kuwait iliyokuwa imevamiwa na kutekwa mwaka uliotangulia lilitimizwa lakini Saddam alisalia mamlakani na aliwageukia Wakurdi na makundi ya Kishia. Mpiga picha Richard Wayman alikuwa amefanya kazi na makundi mengi ya Wakurdi Iraq na Uturuki miaka ya 1980 na aliamua alihitaji kuwa huko. Anakumbuka akifuatilia vita hivyo vya uasi 1991. "Nilikuwa mpiga picha wa kujitegemea na kutoka London nilijaribu kufanya mipango ya kufika maeneo ya Wakurdi Iraq haraka." "Jeshi la Uturuki lilikuwa limefunga mpaka na wanahabari walisubiri katika mji wa mpakani wa Cizre kuruhusiwa kuvuka. Baada ya siku nyingi za kujaribu kupita kisheria bila mafanikio, niliungana na wachumba kutoka kituo cha televisheni cha ZDF TV ya Ujerumani na tukaelekea Silopi - karibu zaidi na mpaka. Baada ya kufanya urafiki na walinzi wa Uturuki tulifanikiwa kuvuka mpaka katika Mto Khabur." "Usiku mmoja kukiwa na giza, tulisukuma mtumbwi wetu mtoni na kuvuka. Upande ule mwingine, tulikutana na kundi la wapiganaji wa Peshmerga wa Kikurdi ambao walitupeleka hadi ngome yao. Wakurdi walikuwa wana furaha, walikuwa wameuteka mji wenye mafuta mengi wa Kirkuk kutoka kwa wanajeshi wa Saddam. Lakini mambo yalianza kubadilika upesi, siku chache tu baadaye, wanajeshi wa serikali waliungana na kuanza kupigana kukomboa maeneo waliyopoteza. Walisaidiwa na hali kwamba nusu ya vifaru vya wanajeshi waaminifu kwa Saddam wa Republican Guard walikuwa wamefanikiwa kutoroka vita Kuwait" "Isitoshe, makubaliano ya kusitisha Vita vya Ghuba yalikuwa yamewazuia wanajeshi wa Iraq dhidi ya kutumia ndege za kawaida anga ya nchi hiyo na badala yake kuwataka watumie tu helikopta kwa sababu madaraja yalikuwa yameharibiwa. Mataifa ya muungano yalikuwa yamekubali ombi la Iraq kutumia helikopta ili kusafirisha maafisa wa serikali. Walizitumia kuzima maasi." Wapiganaji wa Kikurdi walijaribu kupunguza kasi ya wanajeshi wa Republican Guard kuwezesha raia kutoroka maeneo ya Wakurdi na kukimbilia Uturuki na Iran lakini walizidiwa nguvu upesi. Nilitoroka na wakimbizi hadi Uturuki baada ya kutembea siku mbili. Wakurdi waliogopa Saddam angetumia silaha za kemikali kama alivyofanya 1988. Ndoto nyingine ya Wakurdi kujipatia uhuru ilizimwa tena. Zaidi ya Wakurdi milioni moja walikimbilia katika mipaka ya Uturuki na Iran wakijaribu kutoroka. Wengi walifia milimani kabla ya majeshi ya muungano ulioongozwa na Marekani kutengeneza kambi na maeneo salama upande wa Iraq." Picha zote na Richard Wayman

Sunday, April 3, 2016

Matokeo EPL

Leicester waliimarisha nafasi yao ya kutwaa kombe lao la kwanza la ligi kuu ya Uingereza EPl walipoibana Southampton kwa bao moja kwa nunge. Nahodha wa The Foxes Wes Morgan alitumia vyema pasi safi ya Christian Fuchs na kuiweka Leicester alama 7 kileleni mwa jedwali la ligi kuu huku wakiwa wamesalia na mechi 6 kukamilisha msimu huu kwa kishindo. Vijana wa Claudio Ranieri wanaweza kunyanyua kombe la msimu huu iwapo watashinda mechi nne kati ya 6 zilizosalia. Hata hivyo matokeo ya leo yalikuwa ya kipekee kwa nahodha huyo wa Leicester City kwani bao hilo ndilo lililokuwa bao la kwanza la Morgan msimu huu. Southampton watajilaumu wenyewe kwani Sadio Mane kwa wakati mmoja alionekana kuwa fursa nzuri ya angalau kusawazisha hususan baada ya kummwaga Kasper Schmeichel, lakini kombora lake likazimwa na Danny Simpson. Leicester waliendeleza msururu mpya wa ushindi wa bao moja kwa nunge katika mechi 5 kati ya 6 za hivi punde. Matokeo ya wapinzani wao wakuu Tottenham ya sare dhidi ya Liverpool siku ya Jumamosi bila shaka liliwapatia motisha kujikakamua hii leo. Pombe au kitumbua kwa kila shabiki wa Leicester Licha ya kichapo hicho ugenini,Southampton wamesalia katika nafasi ya saba. Awali mashabiki wote walioshuhudia mechi hiyo walipewa kopo la pombe au kaimati kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya mmiliki wa klabu hiyo. Katika mechi nyengine iliyokuwa ikitazamiwa na wengi, bao la Anthony Martial lilitosha kuipa Manchester United ushindi muhimu waliohitaji dhidi ya vibonde wao wa jadi Everton. Katika hafla ya kuadhimisha nyota wao wa zamani Sir Bobby Charlton, vijana wa kocha van Gaal walihitaji ushindi na alama tatu ilikuiweka hai matumaini yao ya kumaliza katika nafasi 4 za kwanza katika EPL. Na baada ya kukosa bao katika kipindi cha kwanza, Man united walirejea kutoka mapumzikoni kwa kishindo. Martialalitumia vyema pasi safi ya Tim Fosu-Mensah na kuiacha Everton ikijiliwaza baada ya kupoteza mechi yao ya tatu mfululizo katika ligi kuu ya Uingereza. Phil Jagielka alikosa nafasi nzuri ya kichwa na kisha kombora lililokolewa na kipa David De Gea. Kufuatia ushindi huo muhimu vijana wa Van Gaal sasa wapo alama 1 tu nyuma ya timu inayorodhoshwa ya nne Manchester City.

Rais magufuli akutana na raila odinga

Magufuli akutana na Raila Odinga Rais wa Tanzania John Magufuli amekutana na kiongozi wa mrengo wa upinzani Kenya, aliyekuwa waziri mkuu Bw Raila Odinga, aliyemtembelea mapumzikoni katika kijiji cha Kilimani, wilaya ya Chato katika mkoa wa Geita kaskazini magharibi mwa Tanzania. Bw Odinga amesema: "Nimekuja kupumzika na nimekuja na Mama na Mtoto wangu wa kike (Winnie Odinga), na vilevile kuja kutoa pongezi kwa ndugu yangu kwani tangu achaguliwe sijakuja hapa Chato, na nilisema siendi Dar es Salaam nitakuja hapahapa Chato". bbcswahili.com Bw Odinga alikuwa miongoni mwa viongozi waliompongeza Dkt Magufuli baada yake kuchaguliwa kuwa rais. http://www.bbc.com/swahili/ medianuai/2015/10/151029_raila_odi nga_matokeo_magufuli Yesterday at 7:07pm · Publi