Monday, June 13, 2016

Soka

kTETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 13.06.2016 Manchester United wapo tayari kutoa pauni milioni 79 kumsajili kiungo wa Paris St-Germain, Marco Verratti (Corriere dello Sport, via Daily Star), Zlatan Ibrahimovic ameahidi kutaja klabu anayokwenda "hivi karibuni" huku tetesi zikiendelea kuashiria kuwa ni Old Trafford (Daily Express), Pep Guardiola anataka kuwasajili John Stones, 22, wa Everton na Aymeric Laporte, 22, katika uhamisho utakaogharimu takriban pauni milioni 85 (Manchester Evening News), Liverpool wametoa pauni milioni 9.5 kumtaka kiungo wa Udinese Piotr Zielinski, 22 (Guardian), Liverpool wanapanga kumfuatilia beki wa River Plate Gabriel Mercado, baada ya meneja Jurgen Klopp kumtazama mchezaji huyo akiichezea Argentina kwenye michuano ya Copa America (Sunday People), Tottenham wanakaribia kukamilisha uhamisho wa kungo wa Southampton, Victor Wanyama kwa pauni milioni 12 (Daily Star), Ronald Koeman anataka kumsajili kipa wa Southampton Fraser Foster mara atakapothibitishwa kuwa meneja mpya wa Everton, Sunday Express). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Sunday, June 12, 2016

Siku ya watu wenye ualbino

Leo ni siku ya Watu Wenye Ualbino "Hii siku ilianza kuanzimishwa miaka mingi iliyopita lakini Umoja Wa Mataifa mwaka juzi ( 2014) uliamua tarehe 13 Juni kila mwaka iwe ni Siku ya kuadhimisha Watu Wenye Ualbino Duniani mara nyingi Umoja wa Mataifa huwa na utaratibu wa kuweka siku maalum kwa makundi fulani ya watu wenye historia kama siku ya Watoto, Mwanamke n.k na sasa suala la watu wenye Ualbino limekuwa ni suala la Haki Za Binadamu, basi Umoja Wa Mataifa wakaamua siku hii iwe maalum kwa ajili ya Watu Wenye Ualbino Duniani kikubwa zaidi ni kwa ajili ya kutoa uelewa kuhakikisha kwamba watu we ye Ualbino wanapata nafasi yao wanayoistahili katika maisha ya kawaida ya mwanadamu, maadhimisho haya yanafanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja" Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Walemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi #PowerBreakFast

Friday, April 15, 2016

Drogba kushtaki gazeti la daily mail

Nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea Didier Drogba amesema atachukua hatua za kisheria dhidi ya gazeti la Daily Mail. Hii ni baada ya gazeti hilo kuchapisha habari zinazodai kwamba kati ya pesa anazokusanya kupitia wakfu wake wa kusaidia jamii, ni chini ya asilimia moja zinazotumiwa kufaa jamii. Gazeti hilo limesema ni £14,115 pekee kati ya £1.7m zinazotolewa na wachezaji nyota na wafanyabiashara ambazo husaidia watoto Afrika. Drogba, 38, ametoa taarifa akisema habari hizo ni za “uongo na za kumharibia sifa”. Drogba anataka kuwa kocha wa Chelsea Drogba hatarejea Chelsea Tume inayodhibiti mashirika ya kusaidia jamii yaliyosajiliwa Uingereza imesema inachunguza “madai ya ukiukaji wa sheria”. Kwenye taarifa yake, Drogba amesema: “Hakuna ulaghai, hakuna ufisadi na hakuna udanganyifu.” Drogba, raia wa Ivory Coast, anayechezea klabu ya Montreal Impact ya Canada kwa sasa amewatuhumu wanahabari wa Daily Mail kwa kuweka hatarini maisha ya maelfu ya watoto wa Afrika. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako

Rais magufuli amfuta kazi mharir wa magazeti ya serikali

AFP Rais wa Tanzania John Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw Gabriel Nderumaki. Bi Tuma Abdallah, ambaye amekuwa mhariri mtendaji msaidizi wa magazeti ya serikali (TSN), ameteuliwa kuwa kaimu. Hakuna maelezo yoyote zaidi yaliyotolewa kuhusu sababu za kutenguliwa kwa uteuzi wa Bw Nderumaki. TSN huchapisha magazeti ya Daily News, Sunday News, habari Leo, Habari Leo Jumapili na Spoti Leo. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako

Friday, April 8, 2016

Kampuni ilitaka kukwepa kodi uganda

Kampuni ya mafuta ilitaka kukwepa kodi Uganda 7 Aprili 2016 Imebadilishwa mwisho saa 17:17 GMT Ushahidi mpya uliotokana na nyaraka zilizofichuliwa za Panama zimefichua jinisi kampuni ya kuchimba mafuta iliyopo Uingereza iliyo na uhusiano na chama tawala ilivyojaribu kukwepa kulipa dola milioni 400 za kodi kwa serikali ya Uganda. Barua pepe zilizofichuliwa na muungano wa waandishi wapelelezi wa kimataifa ICIJ na zilizosambazwa kwa BBC zinaonyesha kuwa kampuni hiyo ilifahamu kuhusu malipo hayo ya kodi yanayohusu uuzaji wa hisa zake katika biashara ya mafuta Uganda. Mapendekezo yaliwasilishwa baadaye ili kukwepa kulipa deni hilo kwa kuhamisha usajili wa kampuni hiyo kutoka Bahamas hadi Mauritius.

Matandika asimamishwa kazi TFF

Matandika asimamishwa kazi TFF Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine amemsimamisha Juma Matandika kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma zinazohusiana na hadhi za wachezaji, shirikisho hilo limesema.

Maasi ya kikurd 1991

wenzako Mpiga picha Richard Wayman anakumbuka akifanya kazi maeneo ya kaskazini mwa Iraq wakati wa maasi ya Wakurdi mwaka 1991. Baada ya zaidi ya mwezi wa mashambulio ya angani na kipindi kifupi cha mashambulio ya ardhi ya wanajeshi wa muungano ulioongozwa na Marekani dhidi ya wanajeshi wa Saddam Hussein, Vita vya Ghuba vya 1991 vilikaribia kumalizika. Lengo la kukomboa Kuwait iliyokuwa imevamiwa na kutekwa mwaka uliotangulia lilitimizwa lakini Saddam alisalia mamlakani na aliwageukia Wakurdi na makundi ya Kishia. Mpiga picha Richard Wayman alikuwa amefanya kazi na makundi mengi ya Wakurdi Iraq na Uturuki miaka ya 1980 na aliamua alihitaji kuwa huko. Anakumbuka akifuatilia vita hivyo vya uasi 1991. "Nilikuwa mpiga picha wa kujitegemea na kutoka London nilijaribu kufanya mipango ya kufika maeneo ya Wakurdi Iraq haraka." "Jeshi la Uturuki lilikuwa limefunga mpaka na wanahabari walisubiri katika mji wa mpakani wa Cizre kuruhusiwa kuvuka. Baada ya siku nyingi za kujaribu kupita kisheria bila mafanikio, niliungana na wachumba kutoka kituo cha televisheni cha ZDF TV ya Ujerumani na tukaelekea Silopi - karibu zaidi na mpaka. Baada ya kufanya urafiki na walinzi wa Uturuki tulifanikiwa kuvuka mpaka katika Mto Khabur." "Usiku mmoja kukiwa na giza, tulisukuma mtumbwi wetu mtoni na kuvuka. Upande ule mwingine, tulikutana na kundi la wapiganaji wa Peshmerga wa Kikurdi ambao walitupeleka hadi ngome yao. Wakurdi walikuwa wana furaha, walikuwa wameuteka mji wenye mafuta mengi wa Kirkuk kutoka kwa wanajeshi wa Saddam. Lakini mambo yalianza kubadilika upesi, siku chache tu baadaye, wanajeshi wa serikali waliungana na kuanza kupigana kukomboa maeneo waliyopoteza. Walisaidiwa na hali kwamba nusu ya vifaru vya wanajeshi waaminifu kwa Saddam wa Republican Guard walikuwa wamefanikiwa kutoroka vita Kuwait" "Isitoshe, makubaliano ya kusitisha Vita vya Ghuba yalikuwa yamewazuia wanajeshi wa Iraq dhidi ya kutumia ndege za kawaida anga ya nchi hiyo na badala yake kuwataka watumie tu helikopta kwa sababu madaraja yalikuwa yameharibiwa. Mataifa ya muungano yalikuwa yamekubali ombi la Iraq kutumia helikopta ili kusafirisha maafisa wa serikali. Walizitumia kuzima maasi." Wapiganaji wa Kikurdi walijaribu kupunguza kasi ya wanajeshi wa Republican Guard kuwezesha raia kutoroka maeneo ya Wakurdi na kukimbilia Uturuki na Iran lakini walizidiwa nguvu upesi. Nilitoroka na wakimbizi hadi Uturuki baada ya kutembea siku mbili. Wakurdi waliogopa Saddam angetumia silaha za kemikali kama alivyofanya 1988. Ndoto nyingine ya Wakurdi kujipatia uhuru ilizimwa tena. Zaidi ya Wakurdi milioni moja walikimbilia katika mipaka ya Uturuki na Iran wakijaribu kutoroka. Wengi walifia milimani kabla ya majeshi ya muungano ulioongozwa na Marekani kutengeneza kambi na maeneo salama upande wa Iraq." Picha zote na Richard Wayman