Monday, June 13, 2016

Soka

kTETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 13.06.2016 Manchester United wapo tayari kutoa pauni milioni 79 kumsajili kiungo wa Paris St-Germain, Marco Verratti (Corriere dello Sport, via Daily Star), Zlatan Ibrahimovic ameahidi kutaja klabu anayokwenda "hivi karibuni" huku tetesi zikiendelea kuashiria kuwa ni Old Trafford (Daily Express), Pep Guardiola anataka kuwasajili John Stones, 22, wa Everton na Aymeric Laporte, 22, katika uhamisho utakaogharimu takriban pauni milioni 85 (Manchester Evening News), Liverpool wametoa pauni milioni 9.5 kumtaka kiungo wa Udinese Piotr Zielinski, 22 (Guardian), Liverpool wanapanga kumfuatilia beki wa River Plate Gabriel Mercado, baada ya meneja Jurgen Klopp kumtazama mchezaji huyo akiichezea Argentina kwenye michuano ya Copa America (Sunday People), Tottenham wanakaribia kukamilisha uhamisho wa kungo wa Southampton, Victor Wanyama kwa pauni milioni 12 (Daily Star), Ronald Koeman anataka kumsajili kipa wa Southampton Fraser Foster mara atakapothibitishwa kuwa meneja mpya wa Everton, Sunday Express). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Sunday, June 12, 2016

Siku ya watu wenye ualbino

Leo ni siku ya Watu Wenye Ualbino "Hii siku ilianza kuanzimishwa miaka mingi iliyopita lakini Umoja Wa Mataifa mwaka juzi ( 2014) uliamua tarehe 13 Juni kila mwaka iwe ni Siku ya kuadhimisha Watu Wenye Ualbino Duniani mara nyingi Umoja wa Mataifa huwa na utaratibu wa kuweka siku maalum kwa makundi fulani ya watu wenye historia kama siku ya Watoto, Mwanamke n.k na sasa suala la watu wenye Ualbino limekuwa ni suala la Haki Za Binadamu, basi Umoja Wa Mataifa wakaamua siku hii iwe maalum kwa ajili ya Watu Wenye Ualbino Duniani kikubwa zaidi ni kwa ajili ya kutoa uelewa kuhakikisha kwamba watu we ye Ualbino wanapata nafasi yao wanayoistahili katika maisha ya kawaida ya mwanadamu, maadhimisho haya yanafanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja" Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Walemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi #PowerBreakFast

Friday, April 15, 2016

Drogba kushtaki gazeti la daily mail

Nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea Didier Drogba amesema atachukua hatua za kisheria dhidi ya gazeti la Daily Mail. Hii ni baada ya gazeti hilo kuchapisha habari zinazodai kwamba kati ya pesa anazokusanya kupitia wakfu wake wa kusaidia jamii, ni chini ya asilimia moja zinazotumiwa kufaa jamii. Gazeti hilo limesema ni £14,115 pekee kati ya £1.7m zinazotolewa na wachezaji nyota na wafanyabiashara ambazo husaidia watoto Afrika. Drogba, 38, ametoa taarifa akisema habari hizo ni za “uongo na za kumharibia sifa”. Drogba anataka kuwa kocha wa Chelsea Drogba hatarejea Chelsea Tume inayodhibiti mashirika ya kusaidia jamii yaliyosajiliwa Uingereza imesema inachunguza “madai ya ukiukaji wa sheria”. Kwenye taarifa yake, Drogba amesema: “Hakuna ulaghai, hakuna ufisadi na hakuna udanganyifu.” Drogba, raia wa Ivory Coast, anayechezea klabu ya Montreal Impact ya Canada kwa sasa amewatuhumu wanahabari wa Daily Mail kwa kuweka hatarini maisha ya maelfu ya watoto wa Afrika. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako

Rais magufuli amfuta kazi mharir wa magazeti ya serikali

AFP Rais wa Tanzania John Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Bw Gabriel Nderumaki. Bi Tuma Abdallah, ambaye amekuwa mhariri mtendaji msaidizi wa magazeti ya serikali (TSN), ameteuliwa kuwa kaimu. Hakuna maelezo yoyote zaidi yaliyotolewa kuhusu sababu za kutenguliwa kwa uteuzi wa Bw Nderumaki. TSN huchapisha magazeti ya Daily News, Sunday News, habari Leo, Habari Leo Jumapili na Spoti Leo. Mshirikishe mwenzako Unavyoweza kumshirikisha mwenzako

Friday, April 8, 2016

Kampuni ilitaka kukwepa kodi uganda

Kampuni ya mafuta ilitaka kukwepa kodi Uganda 7 Aprili 2016 Imebadilishwa mwisho saa 17:17 GMT Ushahidi mpya uliotokana na nyaraka zilizofichuliwa za Panama zimefichua jinisi kampuni ya kuchimba mafuta iliyopo Uingereza iliyo na uhusiano na chama tawala ilivyojaribu kukwepa kulipa dola milioni 400 za kodi kwa serikali ya Uganda. Barua pepe zilizofichuliwa na muungano wa waandishi wapelelezi wa kimataifa ICIJ na zilizosambazwa kwa BBC zinaonyesha kuwa kampuni hiyo ilifahamu kuhusu malipo hayo ya kodi yanayohusu uuzaji wa hisa zake katika biashara ya mafuta Uganda. Mapendekezo yaliwasilishwa baadaye ili kukwepa kulipa deni hilo kwa kuhamisha usajili wa kampuni hiyo kutoka Bahamas hadi Mauritius.

Matandika asimamishwa kazi TFF

Matandika asimamishwa kazi TFF Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine amemsimamisha Juma Matandika kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma zinazohusiana na hadhi za wachezaji, shirikisho hilo limesema.

Maasi ya kikurd 1991

wenzako Mpiga picha Richard Wayman anakumbuka akifanya kazi maeneo ya kaskazini mwa Iraq wakati wa maasi ya Wakurdi mwaka 1991. Baada ya zaidi ya mwezi wa mashambulio ya angani na kipindi kifupi cha mashambulio ya ardhi ya wanajeshi wa muungano ulioongozwa na Marekani dhidi ya wanajeshi wa Saddam Hussein, Vita vya Ghuba vya 1991 vilikaribia kumalizika. Lengo la kukomboa Kuwait iliyokuwa imevamiwa na kutekwa mwaka uliotangulia lilitimizwa lakini Saddam alisalia mamlakani na aliwageukia Wakurdi na makundi ya Kishia. Mpiga picha Richard Wayman alikuwa amefanya kazi na makundi mengi ya Wakurdi Iraq na Uturuki miaka ya 1980 na aliamua alihitaji kuwa huko. Anakumbuka akifuatilia vita hivyo vya uasi 1991. "Nilikuwa mpiga picha wa kujitegemea na kutoka London nilijaribu kufanya mipango ya kufika maeneo ya Wakurdi Iraq haraka." "Jeshi la Uturuki lilikuwa limefunga mpaka na wanahabari walisubiri katika mji wa mpakani wa Cizre kuruhusiwa kuvuka. Baada ya siku nyingi za kujaribu kupita kisheria bila mafanikio, niliungana na wachumba kutoka kituo cha televisheni cha ZDF TV ya Ujerumani na tukaelekea Silopi - karibu zaidi na mpaka. Baada ya kufanya urafiki na walinzi wa Uturuki tulifanikiwa kuvuka mpaka katika Mto Khabur." "Usiku mmoja kukiwa na giza, tulisukuma mtumbwi wetu mtoni na kuvuka. Upande ule mwingine, tulikutana na kundi la wapiganaji wa Peshmerga wa Kikurdi ambao walitupeleka hadi ngome yao. Wakurdi walikuwa wana furaha, walikuwa wameuteka mji wenye mafuta mengi wa Kirkuk kutoka kwa wanajeshi wa Saddam. Lakini mambo yalianza kubadilika upesi, siku chache tu baadaye, wanajeshi wa serikali waliungana na kuanza kupigana kukomboa maeneo waliyopoteza. Walisaidiwa na hali kwamba nusu ya vifaru vya wanajeshi waaminifu kwa Saddam wa Republican Guard walikuwa wamefanikiwa kutoroka vita Kuwait" "Isitoshe, makubaliano ya kusitisha Vita vya Ghuba yalikuwa yamewazuia wanajeshi wa Iraq dhidi ya kutumia ndege za kawaida anga ya nchi hiyo na badala yake kuwataka watumie tu helikopta kwa sababu madaraja yalikuwa yameharibiwa. Mataifa ya muungano yalikuwa yamekubali ombi la Iraq kutumia helikopta ili kusafirisha maafisa wa serikali. Walizitumia kuzima maasi." Wapiganaji wa Kikurdi walijaribu kupunguza kasi ya wanajeshi wa Republican Guard kuwezesha raia kutoroka maeneo ya Wakurdi na kukimbilia Uturuki na Iran lakini walizidiwa nguvu upesi. Nilitoroka na wakimbizi hadi Uturuki baada ya kutembea siku mbili. Wakurdi waliogopa Saddam angetumia silaha za kemikali kama alivyofanya 1988. Ndoto nyingine ya Wakurdi kujipatia uhuru ilizimwa tena. Zaidi ya Wakurdi milioni moja walikimbilia katika mipaka ya Uturuki na Iran wakijaribu kutoroka. Wengi walifia milimani kabla ya majeshi ya muungano ulioongozwa na Marekani kutengeneza kambi na maeneo salama upande wa Iraq." Picha zote na Richard Wayman

Sunday, April 3, 2016

Matokeo EPL

Leicester waliimarisha nafasi yao ya kutwaa kombe lao la kwanza la ligi kuu ya Uingereza EPl walipoibana Southampton kwa bao moja kwa nunge. Nahodha wa The Foxes Wes Morgan alitumia vyema pasi safi ya Christian Fuchs na kuiweka Leicester alama 7 kileleni mwa jedwali la ligi kuu huku wakiwa wamesalia na mechi 6 kukamilisha msimu huu kwa kishindo. Vijana wa Claudio Ranieri wanaweza kunyanyua kombe la msimu huu iwapo watashinda mechi nne kati ya 6 zilizosalia. Hata hivyo matokeo ya leo yalikuwa ya kipekee kwa nahodha huyo wa Leicester City kwani bao hilo ndilo lililokuwa bao la kwanza la Morgan msimu huu. Southampton watajilaumu wenyewe kwani Sadio Mane kwa wakati mmoja alionekana kuwa fursa nzuri ya angalau kusawazisha hususan baada ya kummwaga Kasper Schmeichel, lakini kombora lake likazimwa na Danny Simpson. Leicester waliendeleza msururu mpya wa ushindi wa bao moja kwa nunge katika mechi 5 kati ya 6 za hivi punde. Matokeo ya wapinzani wao wakuu Tottenham ya sare dhidi ya Liverpool siku ya Jumamosi bila shaka liliwapatia motisha kujikakamua hii leo. Pombe au kitumbua kwa kila shabiki wa Leicester Licha ya kichapo hicho ugenini,Southampton wamesalia katika nafasi ya saba. Awali mashabiki wote walioshuhudia mechi hiyo walipewa kopo la pombe au kaimati kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya mmiliki wa klabu hiyo. Katika mechi nyengine iliyokuwa ikitazamiwa na wengi, bao la Anthony Martial lilitosha kuipa Manchester United ushindi muhimu waliohitaji dhidi ya vibonde wao wa jadi Everton. Katika hafla ya kuadhimisha nyota wao wa zamani Sir Bobby Charlton, vijana wa kocha van Gaal walihitaji ushindi na alama tatu ilikuiweka hai matumaini yao ya kumaliza katika nafasi 4 za kwanza katika EPL. Na baada ya kukosa bao katika kipindi cha kwanza, Man united walirejea kutoka mapumzikoni kwa kishindo. Martialalitumia vyema pasi safi ya Tim Fosu-Mensah na kuiacha Everton ikijiliwaza baada ya kupoteza mechi yao ya tatu mfululizo katika ligi kuu ya Uingereza. Phil Jagielka alikosa nafasi nzuri ya kichwa na kisha kombora lililokolewa na kipa David De Gea. Kufuatia ushindi huo muhimu vijana wa Van Gaal sasa wapo alama 1 tu nyuma ya timu inayorodhoshwa ya nne Manchester City.

Rais magufuli akutana na raila odinga

Magufuli akutana na Raila Odinga Rais wa Tanzania John Magufuli amekutana na kiongozi wa mrengo wa upinzani Kenya, aliyekuwa waziri mkuu Bw Raila Odinga, aliyemtembelea mapumzikoni katika kijiji cha Kilimani, wilaya ya Chato katika mkoa wa Geita kaskazini magharibi mwa Tanzania. Bw Odinga amesema: "Nimekuja kupumzika na nimekuja na Mama na Mtoto wangu wa kike (Winnie Odinga), na vilevile kuja kutoa pongezi kwa ndugu yangu kwani tangu achaguliwe sijakuja hapa Chato, na nilisema siendi Dar es Salaam nitakuja hapahapa Chato". bbcswahili.com Bw Odinga alikuwa miongoni mwa viongozi waliompongeza Dkt Magufuli baada yake kuchaguliwa kuwa rais. http://www.bbc.com/swahili/ medianuai/2015/10/151029_raila_odi nga_matokeo_magufuli Yesterday at 7:07pm · Publi

Tuesday, March 29, 2016

Mshukiwa wa brussels aachiwa huru

aachiwa huru Afisi ya kiongozi wa mashtaka nchini Ubelgiji imemuachilia huru mshukiwa mkuu wa mashambulio ya bomu yaliyotokea juma lililopita jijini Brussels. Kingozi wa mashtaka ya umma anasema hakuna ushahidi wa kuthibitisha kuwa mtu anayetambuliwa kama Faycal C ndiye mshukiwa mkuu aliyenaswa na kamera fiche (CCTV) katika eneo lililoathirika. Afisi hiyo inasema hadi kufikia sasa hizo zilikuwa ni madai tu dhidi ya bwana huyo. Faycal C alikamatwa baada ya mtu kuielezea polisi kuwa alimshuku kuwa ndiye aliyeonekana katika picha fiche CCTV katika uwanja wa ndege wa Zaventem muda mchache kabla ya mlipuko huo uliosababisha maafa makubwa. Kufuatia kauli hiyo polisi wamechapisha upya picha za mshukiwa aliyeonekana akiandamana na washambuliaji wa kujitolea mhanga akiwa amevalia kofia. Image Image Kufuatia kauli hiyo polisi wamechapisha upya picha za mshukiwa aliyeonekana akiandamana na washambuliaji Kauli hiyo ya afisi ya kiongozi wa mashtaka imetupilia mbali matumaini ya kumkamata mshukiwa halisi aliyekwepa kutoka eneo la tukio baada ya shambulizi lililoua zaidi ya watu 35. Ibaada ya makumbusho imeratibiwa kufanyika usiku kutwa katika kanisa kuu mjini Brussels.

Saturday, March 26, 2016

Wkb

****Worth Reading**** Great advice from the Richest person in China Mr. Jack Ma. Jack Ma says, "Please tell your children that the world is changing every day and no one is going to wait for you in the past. When lighter was invented, matches slowly disappeared. When calculator was created, abacus was to fade away. When digital camera was designed, the market of negative film no longer existed. When direct market selling/internet-based selling arises, traditional marketing declines. When smartphone with 4G (wireless internet access) was introduced to the world, you no longer need to turn on your computer at home. When WeChat and WhatsApp (mobile text/voice/video messaging) are developed, traditional text messaging is no longer as popular as before. Let's not to blame "Who took over Whose business." It's only because people are more adjustable and adaptable to new ideas and changes in the world. Someone asks Jack Ma, "What is your secret for success?" He says, "Really simple...I am doing (action) while you're only watching." Please remember that the world keeps changing every day. If you don't change, you'll be left behind. You reap what you sow with your time. If you spend time to drink, you may become an alcoholic. If you spend time to complain, you may become a blamer. If you spend time to beautify yourself, you may become a pretty girl/handsome guy. If you spend time to stay healthy, you may enjoy a healthy good life. If you spend time to be picky, you may become a 'mean' person. If you spend time to learn, you may gain wisdom. If you spend time with your family, you may foster a warm and loving relationship with your loved ones.

Friday, March 25, 2016

Wkb

Waholanzi walivyonaswa wakisafirisha Tumbili 61, uwanja wa ndege KIA. VYOMBO vya ulinzi na usalama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) vimefanikiwa kuwanasa wafanyabiashara wawili ndugu, raia wa Uholanzi wakiwa katika harakati ya kusafirisha wanyama Hai 61,aina ya Tumbili kuelekea nchini Armenia. Wanyama hao wakiwa kwenye makasha sita tofauti ya kuhifadhia wanyama walikuwa wasafirishwe kwa ndege maalumu ya mizigo yenye namba EW/364G iliyosajiliwa nchini Belarus kupitia kampuni ya Arusha Freight Limited ya jijini Arusha. Raia hao wa Uholanzi waliokamatwa juzi majira ya saa 1:30 jioni katika uwanja wa ndege wa KIA wametambulika majina yao kuwa ni Arten Vardanian (52) aliyekuwa na hati ya kusafiria yenye namba NWF8CKJR8 na Edward Vardanian (46) aliyekuwa na hati ya kusafiria namba NY969P96.

Wkb

Zaidi ya watu 150 wajitokeza kuhakiki silaha zao. Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Kamishna wa Polisi Diwani Athumani amesema hadi kufikia sasa zaidi ya watu 150 wamejitokeza kuhakiki wa silaha zao, katika hatua ya kutii agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. “Baada ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kufanya uhakiki wa silaha zake hivi karibuni, watu zaidi ya 150 wakiwemo viongozi mbalimbali waliopo Serikalini, Viongozi wastaafu, Mabalozi wa nchi mbalimbali, wafanyabiashara na wabunge wamejitokeza kuhakiki silaha zao, na wengine wameonesha nia ya kufanya hivyo, hata hivyo tusingependa kutaja majina yao kwa sababu za kiusalama” amesema Kamishna wa Polisi Athumani

Wednesday, March 23, 2016

Wkb

Mshukiwa aliyekuwa akisakwa sana kuhusiana na mashambulio ya Brussels amekamatwa na maafisa wa usalama, vyombo vya habari Ubelgiji vimeripoti. Baadhi ya vyombo vya habari limetaja jina lake kuwa Najim Laachraoui. Wadadisi wanasema Laachraoui anaaminika kuwa mtaalamu wa kuunda mabomu. Alionekana kwenye picha ya kamera za usalama uwanja wa ndege akiwa pamoja na washukiwa wawili ambao inadaiwa walijilipua wakati uwanja wa ndege wa Zaventem. Alikuwa tayari anatafutwa na polisi kuhusiana na mashambulio ya Paris mwaka jana. Ripoti za kukamatwa kwake bado hazijathibitishwa na maafisa wa usalama. Taarifa za awali zilikuwa zimewatambua washukiwa walioonekana naye kwenye uwanja wa ndege kuwa ndugu wawili, Brahim na Khalid El Bakraoui. Watu 34 walifariki na zaidi ya 250 kujeruhiwa kwenye mashambulio mawili yaliyotokea katika uwanja huo wa ndege wa Zaventem na kituo cha treni cha Maelbeek. Kundi linalojiita Islamic State limedai kutekeleza mashambulio hayo. Bendera zinapepea nusu mlingoti nchini Ubelgiji. Taifa hilo limetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

Tuesday, March 22, 2016

Wkb

#KutokaMagazetini - MWANDISHI ALIYETOWEKA, APATIKANA. Siku tatu baada ya mwandishi wa Mwananchi na DW, Salma Said kutoweka, jana alipatikana baada ya kukutwa katika Hospitali ya Regency ya jijini hapa na kupelekwa kituo kikuu cha polisi kuhojiwa. Habari zilizopatikana jana jioni na kuthibitishwa na mumewe, Ali Salim Khamis na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi, Simon Siro zilisema Salma alisajiliwa jana mchana katika hospitali hiyo. Ali aliyekuwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, alisema kwa ufupi kuwa amepata taarifa hizo na kufika Dar es Salaam kuzifuatilia. Kamanda Siro alisema ni kweli Salma amepatikana na ametumwa mkuu wa upelelezi wa kanda hiyo kumfuata hospitali ampeleke kituoni kwa mahojiano. Mpaka tunakwenda mitamboni Salma alikuwa anahojiwa. Awali, wadau wa habari waliungana na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), kueleza hofu yao kutokana na kutoweka kwa mwandishi wa habari, Salma Said na kuvitaka vyombo vya dola kulitafutia ufumbuzi wa haraka suala hilo. Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na MwanaSpoti, Francis Nanai alisema wanaendelea kufuatilia kwa makini suala hilo. “Taarifa za kutoweka kwa Salma zilitufikia Ijumaa mchana Machi 18, 2016 kupitia kwa mume wake, mpaka sasa hakuna taarifa yoyote inayoonyesha ni nani au chombo gani kinamshikilia au kumhifadhi, hali hii inatutia wasiwasi mkubwa kama kampuni na wadau wa habari nchini,” alisema Nanai. Wakati huo huo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika tamko lake ililolitoa jana ilieleza kuwa kutekwa kwa mwanahabari huyo kumezua maswali mengi kwa wananchi, familia yake, wadau na wanahabari wa ndani ya nchi na wale wa jumuia za kimataifa. “Kutekwa kwa Salma kunatokana na kazi yake ya uanahabari, ndiyo maana ushahidi wa awali uliopatikana kwa njia ya ujumbe wa sauti ukiwa na sauti inayoaminika kuwa ni yake, ulieleza wazi kutekwa kwake kunatokana na yeye kuripoti dosari zinazoendelea katika uchaguzi wa marudio Zanzibar,” alisema Joseph Mbilinyi, Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wa Kambi ya Upinzani. #Mwananchi