Thursday, August 17, 2017

Tetesi za soka

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 18.08.2017
Manchester United wanataka kumsajili kiungo wa Monaco Thomas Lemar. (Daily Record)

Manchester United bado wana matumaini ya kukamilisha usajili wa Ivan Perisic. (Mirror)

Tottenham wamefikia makubaliano ya kimsingi ya kumsajili Davinson Sanchez, 21, kutoka Ajax kwa pauni milioni 28 na milioni 14 zaidi kama marupurupu. (Independent)

Manchester City wapo tayari kuwapa West Brom pauni milioni 22 ili kumsajili nahodha wao Jonny Evans, 29, baada ya dau la pauni milioni 18 kukataliwa, na watampa mara mbili ya mshahara wa pauni 75,000 kwa wiki anaolipwa sasa. (Mirror)

Dau la Chelsea la pauni milioni 62 kumtaka beki wa Juventus Alex Sandro, limekataliwa. (Mirror)

Chelsea wanajiandaa kumuuza Diego Costa kwa hasara. (Sun)

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Robert Fernandez amesema itakuwa “vigumu” kumsajili kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, kwa sababu hana kipengele cha uhamisho kwenye mkataba wake. (Liverpool Echo)

Barcelona “watapigana” mpaka siku ya mwisho ya usajili ili kumsajili Philippe Coutinho kutoka Liverpool. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, amesema hatorudi Stamford Bridge na anataka kujiunga na Atletico Madrid. (Telegraph)

Everton huenda wakamtaka Diego Costa kwa mkopo. (Sun)

Beki wa Tottenham Kevin Wimmer, 24, anazungumza na Stoke City kuhusu uhamisho wake wa pauni milioni 15. (Telegraph)

Stoke City pia wanataka kumsajili Kevin Wimmer kutoka Spurs. (Stoke Sentinel)

Beki wa Arsenal Gabriel, 26, anakaribia kujiunga na Valencia kwa pauni milioni 10. (Evening Standard)

Paris Saint-Germain bado wanataka kumsajili kiungo mkabaji wa Monaco, Fabinho, 23. (L’Equipe)

Kiungo wa PSG Blaise Matuidi, 30, amekamilisha vipimo vya afya Juventus, lakini timu hizo mbili bado hazijakubaliana jinsi ada ya uhamisho itakavyolipwa, huku meneja wa PSG Unai Emery akisema hakutaka kumuuza mchezaji huyo. (Le Parisien)

Wakurugenzi wa Borussia Dortmund wamesema Barcelona “hata hawapo karibu” katika kufikia dau la mshambuliaji wake Ousmane Dembele, 20. (Kicker)

Fiorentina wamemwambia mshambuliaji wake Nikola Kalinic, 29, anayenyatiwa na AC Milan kuwa atapigwa faini kwa kutotokea mazoezini siku ya Alhamisi. (Sun)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumaa Kareem.

No comments:

Post a Comment