Sunday, July 30, 2017

Tetesi za soka

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 30.07.2017
Baba yake Neymar ameiomba PSG kusubiri kuanza mazungumzo rasmi ya uhamisho wa pauni milioni 450 wa mwanae hadi baada ya Julai 31, tarehe ambayo atapata bakshishi yake ya pauni milioni 23.3 kutoka kwa Barcelona ya kumshawishi Neymar kusaini mkataba mpya mwaka jana Oktoba. (Sunday Times)

Barcelona watawashtaki Paris Saint-Germain kwa UEFA kwa kukiuka kanuni za fedha (FFP) iwapo PSG watatoa dau la pauni milioni 197 kutengua kifungu cha usajili cha Neymar. (ESPN)

Iwapo Neymar, 25, ataondoka Barcelona na kujiunga na PSG, Barca huenda wakaamua kumchukua mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoinne Griezmann, 26 kuziba pengo. (Marca)

PSG wakikamilisha usajili wa Neymar, watapanda dau la pauni milioni 35 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, 28 kutoka Arsenal. (Sunday Express)

Philippe Coutinho, 25, atamuomba meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kumruhusu ajiunge na Barcelona. Iwapo Coutinho ataondoka, Klopp atataka kumsajili winga wa Borussia Dortmund Christian Pulisic. (Sunday Mirror)

Meneja wa RB Leipzig amesema kiungo Naby Keita, 22,  anayenyatiwa na Liverpool ana asilimia 100 ya kubakia katika klabu hiyo ya Bundesliga. (Observer)

Uhamisho wa kiungo Nemanja Matic, 28, kutoka Chelsea kwenda Manchester United umekwama kutokana na kutofautiana kuhusu malipo ya marupurupu kwa Chelsea katika sehemu ya mkataba huo. (Sun on Sunday)

Manchester United huenda wakakamilisha usajili wa Nemanja Matic, 28, kutoka Chelsea mwishoni mwa wiki ijayo. (Daily Mail)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho atasubiri hadi msimu ujao kutoa pauni milioni 90 kumsajili Gareth Bale, 28, kutoka Real Madrid. (Sunday Express)

Meneja wa Inter Milan Luciano Spalletti “anapinga vikali” hatua ya kuondoka kwa winga Ivan Perisic, 28, ambaye amehusishwa na Manchester United. (Observer)

Manchester United wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 48 wa Ivan Perisic kutoka Inter Milan. (Daily Star)

Kiungo wa Manchester United Marouanne Fellaini, 29, amekubali mkataba wa kujiunga na Galatasaray ya Uturuki. (Ajansspor)

Manchester United wamehusishwa na kumtaka kiungo wa Anderlecht Leander Dendocker, 22, huku mkurugenzi wa klabu hiyo akisema timu ikija na dau la euro milioni 25-35, itakuwa vigumu kukataa. (Het Belang van Limburg)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, yuko tayari kuwasilisha maombi ya rasmi ya uhamisho ili kulazimisha uhamisho wake kwenda Manchester City. (Sunday Mirror)

Manchester City wamerejea katika orodha ya UEFA ya timu zinazomulikwa kwa kukiuka kifungu cha fedha (FFP) baada ya kutumia pauni milioni 220 kusajili msimu huu. (Sunday Telegraph)

Kiungo wa Everton Ross Barkley, 23, anawindwa na timu sita za EPL, huku Tottenham na Manchester City wakiongoza mbio za kutaka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa England. (Daily Star Sunday)

Everton wanafikiria kutoa pauni milioni 9 kumsajili beki wa West ham Winston Reid. (Mail on Sunday)

Chelsea wapo tayari kutoa hadi euro milioni 70 kumsajili Alex Sandro. (Calciomercato)

Mkurugenzi wa michezo wa Roma, Monci, anasema klabu yake sasa inatazama kwingine baada ya dau jingine la kumtaka Riyad Mahrez, 26, kukataliwa na Leicester. (Evening Standard)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte atatoa ombi jipya kwa klabu la kununua wachezaji wapya zaidi wiki ijayo baada ya kusema ana wasiwasi wa kufukuzwa kazi. Tayari Chelsea wametumia pauni milioni 130 msimu huu. (Sunday Telegraph)

Newcastle wanataka kumsajili Lucas Perez, 28, wa Arsenal na kumfanya kuwa mshambuliaji mkuu wa klabu hiyo, licha ya mchezaji huyo kutaka kurejea katika klabu yake ya zamani Deportivo La Coruna. (Sun on Sunday)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Tafadhali share tetesi hizi na wapenda soka wote. Nakutakia Jumapili njema.

Wednesday, July 26, 2017

Tetesi za soka

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO 26.07.2017
Mancheter City wanajaribu kuwapiku Real Madrid katika kumsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Daily Mirror)

Manchester City wapo tayari kutoa pauni milioni 160 kumsajili Kylian Mbappe katika harakati za Pep Guardiola kujenga kikosi chake. (ESPN)

Kylian Mbappe ambaye alipachika mabao 15 katika mechi 29 za Ligue 1 msimu uliopita atakataa kwenda Manchester City akitaka kujiunga na Real Madrid. (Daily Star)

Manchester City hawajapanda dau lolote kumtaka Kylian Mbappe, na wala hawana mpango huo, ingawa Pep Guardiola amesema Real Madrid hawana ‘msuli’ mkubwa wa kifedha kama wa City. (Sky Sports)

Real Madrid wamefikia makubaliano na Monaco ya kumsajili Kylian Mbappe kwa euro milioni 180. (Marca)

Kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho anakaribia ’sana’ kujiunga na Barcelona (Mundo Deportivo)

Barcelona wametuma maafisa wake hapa England kujaribu kumsajili Philippe Coutinho, 25, licha ya Liverpool kukataa dau la pauni milioni 72. (Sports)

Liverpool wanasisitiza kuwa Philippe Coutinho hauzwi, lakini Barcelona wapo tayari kupanda dau la pauni milioni 80. (Daily Star)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema timu yake haiogopi ‘kumwaga fedha’ msimu huu huku wakiendelea kumsaka beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26. (Daily Mirror)

Liverpool wanatarajiwa kukamilisha usajili wa Virgil van Dijk kutoka Southampton ifikapo mwisho wa dirisha la usajili. (Sky Sports)

Arsenal hatimaye wanakaribia kumsajili kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21, kwa pauni milioni 45. (Sun)

Arsenal wanafikiria kumsajili kiungo wa Nice, Jean Michael Seri. (L’Equipe)

Arsenal wanakabiliwa na kupata hasara kwa mshambuliaji wake Lucas Perez, baada ya Deportivo La Coruna kutoa pauni milioni 9 kutaka kumsajili mchezaji huyo, 28. (Evening Standard)

Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 25, anataka kubakia London iwapo ataondoka Emirates, huku West Ham ikionekana ni kimbilio lake. (Independent)

Stoke City wanataka kununua wachezaji kadhaa katika wiki chache zijazo, lakini hawana mpango wa kumtaka winga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 23. (Stoke Sentinel)

Kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches, 19, amesema anataka kuondoka Ujerumani huku AC Milan na Manchester United wakimnyatia mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 43. (Independent)

Tottenham wanafikiria kumsajili beki wa Hoffenheim Jeremy Toljan, 22, baada ya mazungumzo ya kumsajili beki Ricardo Pereira, 23, wa Porto kukwama. (Daily Mail)

Everton wamepanda dau la pili la pauni milioni 45 kutaka kumsajili kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson. (The Telegraph)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na wiki njema.

Tuesday, July 25, 2017

Tetesi za soka

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 25.07.2017
Meneja wa Chelsea Antonio Conte atakabidhiwa pauni milioni 150 zaidi za usajili huku akitaka kumchukua Virgil van Dijk, 26, kutoka Southampton na beki wa kushoto wa Juventus, Alex Sandro, 26. (Daily Mirror)

Kitita cha usajili cha Chelsea huenda kikafikia cha Manchester City cha pauni milioni 218. (Times)

Chelsea huenda wakatumia fedha zaidi wakati Antonio Conte akitaka kumsajili Antonio Candreva, 30, kutoka Inter Milan na pia mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente, 32 na pia kiungo wa Everton Tom Davies, 19. (Sun)

Chelsea vilevile wanataka kuwasajili Cedric Soares na Ryan Bertrand kutoka Southampton baada ya kumkosa Danilo na Benjamin Mendy. (Daily Star)

Chelsea wapo tayari kulipa euro milioni 40 za kutengua kifungu cha usajili ili kumchukua Sergi Roberto kutoka Barcelona. (Sport)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, yuko tayari kupunguziwa mshahara ili aweze kujiunga na Manchester City. Sanchez anapenda kwenda City kuliko Bayern Munich, PSG au Juventus. (Independent)

Arsenal na Liverpool huenda wakaamua kumsajili Karim Benzima, 29, iwapo Real Madrid wataamua kumuuza ili kumchukua Kylian Mbappe. Hata hivyo Real huenda wakamtumia Benzima pia kama chambo kwa Monaco ili kupunguza bei ya Mbappe. (Don Balon)

Liverpool wanamfuatilia kiungo wa kimataifa wa Poland, Sebastian Szymanski, 18, ambaye anachezea Legia Warsaw. (Polska Times)

Liverpool wamewaambia Crystal Palace watoe pauni milioni 30 kumchukua beki Mamadou Sakho, 27, na kuwa hawatokubali kumtoa kwa mkopo tena. (Daily Mirror)

Liverpool wametoa dau la pauni milioni 74 kumtaka kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22, baada dau mbili za awali kukataliwa. (Daily Star)

Emre Can amefikia makubaliano ya maslahi binafsi na Juventus na anasubiri dau rasmi la pauni milioni 30.4 kutolewa ili kufanikisha uhamisho wake. (TMW)

Manchester City wamedhamiria kufunga dirisha la usajili kwa kumwaga fedha kwa kumsajili Alexis Sanchez, 28, au Kylian Mbappe, 18. Pep Guardiola hatoridhika mpaka ampate Sanchez anayedhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 50 au Mbappe ambaye ada yake inaweza kufika pauni milioni 100. (Daily Mail)

Roma wametoa pauni milioni 30 pamoja na marupurupu mengine kumtaka Riyad Mahrez, 26, lakini Leicester wanataka pauni milioni 50. (Daily Mail)

Riyad Mahrez, 26, Huenda akajikuta amebakia Leicester msimu ujao iwapo timu zinazomtaka ikiwemo Arsenal zitashindwa kutoa pauni milioni 50 kumsajili. (The Sun)

Everton wana uhakika wa kukamilisha usajili wa kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27, kwa pauni milioni 45, ifikapo siku ya Alhamisi. (Daily Mail)

Manchester United huenda wakamsajili kiungo wa Bayern Munich Renato Sanchez, 19, kwa mujibu wa meneja Carlo Ancelotti, lakini Arturo Vidal, 30, haondoki kwa mabingwa hao wa Bundesliga. (Independent)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho atakataa dau lolote la kumtaka Ashley Young, 32, ambaye Stoke City wamekuwa wakimuulizia. (The Sun)

Galatasaray wanazungumza na Arsenal kuhusu kumsajili kiungo kutoka Misri Mohamed Elneny, 25. (Fotospor)

Paris Saint-Germain wamewapa Barcelona kiungo Marco Verratti pamoja na pauni milioni 90 juu, ili kumsajili Neymar. (Diario Gol)

Kiungo wa Chelsea Mason Hunt, 18, amesaini mkataba mpya wa miaka minne kabla ya kwenda Vitese kwa mkopo. (London Evening Standard)

Marseille wanazungumza na Celtic kutaka kumsajili mshambuliaji Moussa Dembele, 21, kwa pauni milioni 20. (Daily Express)

Borussia Dortmund wanataka kumsajili winga wa Manchester City Jadon Sancho, 17. (ESPN)

Winga wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele anataka kwenda Real Madrid baada ya kukata tamaa ya kusubiri dau kutoka kwa Barcelona. (Don Balon)

Mshambuliaji wa Arsenal Lucas Perez, 28, anataka kuondoka Emirates baada ya kuhisi “kusalitiwa” kufuatia namba yake ya jezi, 9, kupewa Alexandre Lacazette. (La Voz de Galicia)

Tottenham wamemkosa beki Juan Foyth, 19, ambaye anakaribia kujiunga na Paris Saint-Germain. (Squawka)

Swansea wamekubaliana na Manchester City kuhusu usajili wa Wilfried Bony, lakini wana wasiwasi na madai ya mshahara wa pauni 130,000 kwa wiki. Swansea wanahitaji mshambuliaji kutokana na uwezekano wa Fernando Llorente kuondoka kwenda Chelsea. (Wales Online)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na wiki njema.

Sunday, July 23, 2017

Tetesi za soka

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 23.07.2017
Barcelona wapo tayari kutoa pauni milioni 80 kumtaka Philippe Coutinho, 25, kutoka Liverpool. (Sunday Mirror)

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi, 30, ameiambia klabu yake kumsajili mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, 23. (Don Balon)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema Coutinho “ametulia” Liverpool baada ya klabu hiyo kuzungumza naye kufuatia hatua ya Barcelona kumtaka. (ESPN FC)

Liverpool hatimaye wamefikia makubaliano na RB Leipzig ya pauni milioni 75 ili kumsajili Naby Keita. (Winner Sports)

Meneja wa Arsenal amekanusha taarifa kuwa Alexis Sanchez, 28, anakaribia kuhamia Paris Saint-Germain kwa pauni milioni 70. (Standard)

Alexis Sanchez anataka mshahara wa pauni 500,000 kwa wiki kutoka Paris Saint-Germain, huku akikaribia kuhamia Paris. (The Mirror)

Liverpool na Arsenal wameonesha dalili za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Lucas Vasquez. (Diario Madridista)

Chelsea wanapanga kuzungumza na Arsenal kuhusiana na Alex Oxlade-Chamberlain, 23. (Sky Sports)

Chelsea wanamfuatilia winga wa Montreal Impact Ballou Jean-Yves Talba, baada ya Didier Drogba kuwaambia kuhusu mchezaji huyo. (Sun)

Manchester United wana uhakika wa kumsajili kiungo wa Chelsea Nemanja Matic, 28, baada ya kumkosa Eric Dier, 23, wa Tottenham. (Guardian)

Mipango ya Manchester United kutaka kumsajili kiungo wa PSG, Marco Verratti, 24, kwa pauni milioni 60 imesitishwa kwa muda baada ya PSG kusema inamtaka Anthony Martial, 21. (Sunday Mirror)

Jose Mourinho amesema “ana uhakika” David de Gea atabakia Manchester United msimu huu, baada ya Real Madrid kushindwa kutumia nafasi ya kumsajili kipa huyo. (Sky Transfer Centre)

Manchester United sasa wamemgeukia kiungo wa Bayern Munich, Arturo Vidal, wakati wakitafuta kiungo mpya. (Daily Star)

Beki wa Manchester United Matteo Darmian, 27, amesema haendi popote licha ya taarifa kumhusisha na kurejea Italy. (Press Association)

Real Madrid wametengeneza orodha ya washambuliaji inayowataka, ikiwa watamkosa Kylian Mbappe. Miongoni mwao ni Marcus Rashford wa Manchester United, Pierre Emerick-Aubameyang wa Borussia Dortmund na Timo Werner wa RB Leipzig. (Diario Gol)

Real Madrid watamsajili mshambuliaji wa Ajax Kasper Dolberg pamoja na Domenico Berardi wa Sassuolo, iwapo watamkosa Kylian Mbappe. (Marca)

Real Madrid wamewaambia Monaco watawapa Karim Benzima kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Kylian Mbappe. (The Sun)

Chelsea wamemuulizia winga wa Inter Milan Antonio Candreva, ili kuogeza ushindani Stamford Bridge. (the Sun)

Kiungo wa Manchester City Kevin de Bruyne, 26, amesema ana matumaini klabu yake itanunua mabeki wengine kadhaa msimu huu. (Manchester Evening News)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na Jumapili njema.

Friday, July 21, 2017

Tetesi za soka

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 21.07.2017
Dau la Manchester City la pauni milioni 44.5 la kumtaka beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 23, limekataliwa. Monaco wanataka pauni milioni 54. (Daily Mail)

Manchester City wapo tayari kumfanya Benjamin Mendy, 23, kuwa beki aghali zaidi duniani kwa kumsajili kutoka Monaco. (L’Equipe)

Manchester City watakamilisha usajili wa Danilo, 26, kutoka Real Madrid siku ya Ijumaa. (Marca)

Beki wa Manchester City Aleksander Kolarov anakaribia kujiunga na Roma, kwa mujibu wa meneja wake Pep Guardiola. (Sky)

Barcelona wamewasilisha dau la pauni milioni 72 kumtaka kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, lakini Liverpool wanatarajiwa kutupilia mbali dau hilo. (Daily Mail)

Liverpool wamesema Barcelona wanapoteza muda wao kutaka kumsajili Philippe Coutinho, 25. (Liverpool Echo)

Juventus wanataka kuimarisha kiungo chao kwa kumsajili Emre Can kutoka Liverpool. (Gianluca Dimarzio)

Arsenal wana uhakika kuwa kiungo wao Mesut Ozil, 28, atasaini mkataba mpya kubakia Emirates. (Sun)

Manchester United sasa wameelekeza nguvu zao kumtaka beki wa kulia wa Paris Saint-Germain, Serge Aurier, 24, kutokana na kusuasua kwa mipango ya kumsajili Fabinho, 23, kutoka Monaco. (Independent)

Meneja wa PSG Unai Emery amethibitisha kuwa Serge Aurier anataka kuondoka Paris msimu huu. (L’Equipe)

Manchester United wanataka kuwazidi kete AC Milan katika kumsajili Renato Sanches kutoka Bayern Munich. (The Guardian)

Manchester United bado hawajafikia dau wanalotaka Inter Milan katika kumsajili Ivan Perisic, 28. (Daily Mirror)

Jose Mourinho ameitaka klabu yake ya Manchester United kumsaidia kusajili mchezaji mmoja tu zaidi “haraka iwezekanavyo”. (Sky Sports)

Wolfsburg wameulizia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial. (Kicker)

Diego Costa huenda akacheza kwa mkopo AC Milan, wakati akisubiri kuhamia Atletico Madrid. (Don Balon)

Chelsea wapo tayari kumuuza Diego Costa kwenda Atletico Madrid kwa pauni milioni 44, na sio pauni milioni 25 zilizotolewa na Atletico. (Independent)

Alexis Sanchez, 28, amefikia makubaliano na Paris Saint-Germain, na klabu hiyo ya Ufaransa itapanda dau la pauni milioni 45. Kinachosubiriwa ni kauli ya Arsene Wenger. (Sun)

Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 25, yuko tayari kwenda West Ham, iwapo klabu hiyo itafikia makubaliano kuhusu ada ya uhamisho. (Daily Star)

Arsenal wamekataa dau la pauni milioni 16, la kumsajili beki wake Callum Chambers. Arsenal wanataka pauni milioni 20. (Daily Telegraph)

Tottenham wametaka kufahamishwa msimamo wa Riyad Mahrez, lakini Leicester watalazimika kupunguza bei ya pauni milioni 50, kama watamuuza kwenda White Hart Lane. (Standard)

Wachezaji wa Leicester City wapo tayari ‘kumhamasisha kwa lazima’ Riyad Mahrez ikiwa hatajituma kwa asilimia 100, amesema kiungo Andy King. (Leicester Mercury)

Meneja wa Leicester City Craig Shakespeare amethibitisha kuwa wamekataa dau kutoka Roma la kumtaka Riyad Mahrez. (Sky Transfer Centre)

Arsenal na Tottenham zinamnyatia winga kinda wa Manchester City Jadon Sancho, 17. (Independent)

Mshambuliaji wa Stoke City, Marco Arnautovic, 28, atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi West Ham baada ya kukamilisha vipimo vyake vya afya siku ya Ijumaa. (Daily Express)

Torino wanataka AC Milan itoe euro milioni 50 pamoja na M’Baye Niang, Gabriel Paletta na Manuel Locatelli, kama wanamtaka Andrea Belotti. (La Stampa)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumaa Kareem.

Thursday, July 20, 2017

Tetesi za soka

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 20.07.2017
Paris Saint-Germain wanajiandaa kuzungumza na Barcelona kuhusu uhamisho wa pauni milioni 196 wa Neymar, 25. (Guardian)

PSG wapo tayari kumpa Neymar pauni milioni 45, za kukubali tu kujiunga nao, na mshahara wa pauni 596,000 kwa wiki (baada ya makato ya kodi) na mkataba wa miaka mitano. (Daily Mail)

Barcelona wanapanga kuzungumza na Monaco kuhusu kumsajili Kylian Mbappe, 18. Barca wanatarajia kupata fedha za kutosha kumsajili Mbappe baada ya kumuuza Neymar, 25. (Daily Mail)

Chelsea wanataka pauni milioni 44 kutoka kwa Atletico Madrid kwa ajili ya Diego Costa, 28, baada ya kukamilisha usajili wa Alvaro Morata, 24, kutoka Real Madrid. (Independent)

Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo amesema hakuna uhakika thabiti iwapo Diego Costa atakwenda Atletico Madrid. (Mirror)

Chelsea, Tottenham na Manchester United huenda zikaingia katika mapambano ya kumgombania kiungo wa Everton Ross Barkley, 23. (The Times)

Liverpool wapo tayari kutoa pauni milioni 70 kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22, baada ya dau la pauni milioni 66 kukataliwa. (Mirror)

West Ham wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier ‘Chicharito’ Hernandez, 29, kutoka Bayer Leverkusen. (Sky Sports)

Arsenal wamewaambia West Ham kuwa watalazimika kutoa pauni milioni 20 ikiwa wanamtaka kiungo Jack Wilshere, 25. (Daily Star)

Paris Saint-Germain wamemtuma mkurugenzi wao wa michezo kwenda London kujaribu kumshawishi Alexis Sanchez, 28, ambaye pia anasakwa na Manchester City. (Sun)

Everton wamepata matumaini zaidi ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30. (The Telegraph)

Kiungo wa Arsenal Mohamed Elneny amekataa kuhamia Leicester City waliokuwa tayari kutoa pauni milioni 10 kumsajili. (The Sun)

Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa Real Madrid Danilo, 26, kwa pauni milioni 26.5. (Guardian)

Manchester city wanakaribia kukamilisha usajili wa beki Benjamin Mendy, 23, kutoka Monaco. (Times)

Manchester United wanahusishwa na kutaka kumsajili kiungo wa Paris Saint-Germain, Marco Verratti, 24, baada ya mchezaji huyo kumfanya Mino Raiola kuwa wakala wake mpya. (Sun)

Manchester United na Chelsea zilitazama uwezekano wa kumsajili Neymar, lakini timu hizo mbili zilikatishwa tamaa na bei ya pauni milioni 196 ya mchezaji huyo, 25, kutoka Brazil. (Independent)

Inter Milan wamewaambia Manchester United lazima wamjumuishe Anthony Martial, 21, katika mkataba wowote utakaohusu uhamisho wa Ivan Perisic, 28. (Independent)

AC Milan wamesema kiungo mshambuliaji wao Suso, 23, anayenyatiwa na Tottenham, hauzwi. (Tuttomercato)

PSG watamuuza kiungo Blaise Matuidi, 30, iwapo dau zuri litatolewa. (L’Equipe)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema.

Saturday, July 15, 2017

Tetesi za soka

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 15.07.2017
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekuwa akimtumia ujumbe mfupi wa maandishi Alexis Sanchez, 28, kujaribu kumshawishi asiondoke Emirates. (Sun)

Mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe ameonesha dalili za kuondoka katika klabu yake hiyo huku Arsenal wakiendelea kumnyatia. (Marca)

Chelsea wana uhakika wa kuwapiku Liverpool katika kumsajili Pierre Emerick-Aubameyang, 28, kutoka Borussia Dortmund, ambao sasa wameanza mazungumzo ya kumtaka Olivier Giroud wa Arsenal. (Daily Mirror)

Nemanja Matic, 28, huenda akajiunga na Juventus baada ya Chelsea kumruhusu kutojiunga na kikosi kinachokwenda China na Singapore kwa ajili ya mechi za kujiandaa na msimu mpya. Diego Costa pia ameachwa. (Guardian)

Arsenal wameonesha dalili za kumtaka Nemanja Matic, na wapo tayari kubadilishana na Alex Oxlade-Chamberlain, 23. (Calcio Mercato)

Kasper Schmeichel, 30, amepata matumaini ya kujiunga na Manchester United baada ya taarifa kuwa Real Madrid wamepanda dau la kumtaka David de Gea, 26. (Daily Mirror)

Manchester United wana uhakika Real Madrid hawataiweza bei ya David de Gea. (ESPN)

Iwapo David de Gea atakwenda Real Madrid, meneja wa Manchester United atataka mchezaji mmoja kutoka Real na huenda akamtaka beki Rafael Varane. (Don Balon)

Kipa namba tatu wa Manchester United, Joel Pereira, 21, ana nafasi ya kuwa namba moja iwapo De Gea ataondoka. (Independent)

Inter Milan huenda wakamuulizia mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial wamchukue kwa mkopo kama sehemu ya mkataba wa United kumsajili Ivan Perisic, 28. (Daily Telegraph)

Tottenham watachuana na Juventus katika kumsajili beki wa Porto Ricardo Pereira, na watatazamiwa kulipa pauni milioni 22, kumchukua mchezaji huyo kuziba pengo la Kyle Walker. (Evening Standard)

Joe Hart anakaribia kukamilisha usajili wake wa pauni milioni 10 kutoka Manchester City kwenda West Ham. (Manchester Evening News)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho hatoishutumu bodi ya klabu kwa kushindwa kumsajili Alvaro Morata. (Daily Express)

Liverpool huenda wakapanda dau la pauni milioni 65 kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22. (Liverpool Echo)

Roma wanajiandaa kupanda dau la pauni milioni 30 kumtaka winga wa Leicester Riyad Mahrez, 26. (Goal)

Meneja wa Birmingham Harry Redknapp anataka kumsajili beki wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Ashley Cole, 36, kutoka LA Galaxy. (Sun)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumamosi njema.

Friday, July 14, 2017

Tetesi

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 14.07.2017
Liverpool na Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, ambaye thamani yake ni pauni milioni 65. (Sun)

Dortmund wamemuambia Aubameyang kuamua anataka kwenda wapi kabla klabu hiyo haijaingia kambini nchini Uswisi Julai 24. (Sun)

Kipa wa Manchester United David de Gea, 26, anataka kujiunga na Real Madrid msimu huu na amemuambia wakala wake Jorge Mendes kufanikisha uhamisho wake. (Don Balon)

Manchester City wapo tayari kutoa pauni milioni 50 kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22. (Daily Mirror)

Chelsea watakamilisha usajili wa kiungo Tiemoue Bakayoko, 22, kutoka Monaco kwa pauni milioni 39.7 katika saa 24 zijazo, ingawa mchezaji huyo atakosa mechi kadhaa za mwanzo kutokana na kuwa majeruhi. (Daily Express)

RB Lepzig wamekataa dau la pauni milioni 57 kutoka Liverpool la kumtaka kiungo Naby Keita, 22. (Bild)

Kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27, atakataa kwenda Leicester kwa sababu anataka kujiunga na Everton. (Leicester Mercury)

West Ham wanakaribia kukamilisha usajili wa mkopo wa kipa wa Manchester City Joe Hart, 30. (Independent)

Newcastle watapewa nafasi ya kumsajili kipa wa West Ham Darren Randolp, ikiwa Joe Hart atakwenda West Ham. (Newcastle Chronicle)

Barcelona wameacha kumfuatilia beki wa Arsenal Hector Bellerin, 22, baada ya klabu hiyo ya Uhispania kufikia makubaliano ya kumsajili Nelson Semedo, 23 kutoka Benfica. (London Evening Standard)

Roma wametoa dau la pauni milioni 29 kumtaka Riyad Mahrez, 26, lakini Leicester wanataka pauni milioni 50. (London Evening Standard)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka uhamisho wa Kyle Walker, 27, kwenda Man City uharakishwe ili wapate fedha za kusajili wachezaji wengine. (Daily Mail)

Tottenham wanatarajia kuziba pengo la Kyle Walker kwa kumsajili beki wa Porto Rocardo Pereira, 23, kwa pauni milioni 22. (Times)

Tottenham wanakaribia kukamilisha usajili wa beki Juan Foyth, 19, kutoka Estudiantes, ambaye atakuwa usajili wa kwanza wa Spurs msimu huu. (ESPN)

Tianjin Quanjian wamempa mkataba wa pauni milioni 26 kwa mwaka, mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24. (Onda Cero)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Ijumaa Kareem.

Thursday, July 13, 2017

Tetesi

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 13.07.2017
Chelsea wameambiwa wanaweza kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, kwa pauni milioni 60 baada ya Tianjin Quanjian ya China kusema haitaki tena kumsajili mchezaji huyo. (Daily Mail)

Borussia Dortmund huenda wakaamua kumfuatilia mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30, ambaye pia anasakwa na Everton, West Ham, Marseille na AC Milan. (Daily Mirror)

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26, amempigia simu meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane na kumuambia hana mpango wa kuondoka Chelsea msimu huu. (Diario Gol)

Chelsea wamefikia makubaliano na Monaco ya kumsajili kiungo Tiemoue Bakayoko, 22, kwa pauni milioni 40 kwa mkataba wa miaka mitano. (RMC)

Meneja wa Chelsea anajiandaa kumuuza kiungo Nemanja Matic, 28, kwa pauni milioni 40. Matic amekuwa akifanya mazoezi peke yake na anataka kuungana na Jose Mourinho Old Trafford. (Daily Telegraph)

Barcelona wanataka kumsajili beki wa Chelsea Cesar Azpilicueta baada ya kushindwa kumpata Hector Bellerin wa Arsenal. (Marca)

Chelsea watawazidi kete Juventus katika kumsajili beki wa kulia wa Real Madrid Danilo, 25, kwa pauni milioni 28. (Daily Mirror)

Mchezaji wa zamani wa Liverpool Danny Murphy amesema klabu hiyo inakaribia kukamilisha usajili wa Virgil van Dijk, 26, kutoka Southampton. (Sports360)

Arsenal wana uhakika dau la pauni milioni 45 litatosha kumsajili winga wa Monaco Thomas Lemar, 21. (Daily Mail)

Arsenal wanataka kumsajili kinda wa West Ham Domingos Quina, 17. (Sky Sports)

Roma wanataka kumsajili winga wa Leicester City Riyad Mahrez, 26. (Sky Italia)

Tottenham wamesema hawatoburuzwa na Manchester United na Manchester City kuhusu usajili wa Eric Dier na Kyle Walker, huku wakikaribia kumsajili beki Juan Foyth, 19, kutoka Estudiantes kwa pauni milioni 9. (Daily Telegraph)

Manchester United wana matumaini ya kukamilisha usajili wa winga wa Inter Milan Ivan Persic, 28, wiki ijayo. (Daily Star)

Manchester United sasa wataelekeza nguvu zao kumsajili kiungo wa Roma Radja Nainggolan, 29, kwa kutoa pauni milioni 40 baada ya Tottenham kukataa dau lolote kuhusu Eric Dier. (Daily Mail)

Leicester City huenda wakaondoa wachezaji sita waliosajiliwa msimu uliopita akiwemo Islam Slimani, 29, na Ahmed Musa, 24, pamoja na kiungo Nampalys Mendy, 25. (Daily Telegraph)

Middlesbrough wamewazidi kete Burnley na Watford katika kumsajili Britt Assombalonga, 24, kwa pauni milioni 14 kutoka Nottingham Forest. (Sun)

West Ham wanafikiria kupanda dau la tatu kumtaka Marco Arnautovic, 28, baada ya dau la pauni milioni 20 kukataliwa na Stoke City. (London Evening Standard)

Watford na Swansea zinamtaka kiungo wa Chelsea Nathaniel Chalobah, 22. (Sun)

Real Madrid wamekata tamaa ya kumpata kipa wa Manchester United David de Gea, 26, msimu huu. (Daily Star)

Manchester City wanakaribia kumsajili kiungo kutoka Brazil Douglas Luiz, 19, anayechezea Vasco da Gama. (ESPN)

Manchester City wanataka kupanda dau la pauni milioni 25 kumtaka beki wa Southampton Ryan Bertrand, 27, baada ya kumkosa Dani Alves aliyesaini PSG. (Daily Mail)

Stoke City watawazidi kete West Brom katika kumsajili beki wa Chelsea Kurt Zouma, 22 kwa mkopo. (Sun)
Fenerbahce ya Uturuki inataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi, 23. (Fanatik)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema.

Tuesday, July 11, 2017

Usajili

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 11.07.2017
Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko, 22, na huenda akasaini mkataba wake kabla ya Jumatatu na kusafiri na timu kwenda Singapore na China (Sky Sports).

Manchester United wanataka kupanda dau zaidi ya la Chelsea na kumsajili Tiemoue Bakayoko kwa pauni milioni 40 (Daily Mail).

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho pia anataka klabu hiyo kutoa dau la pauni milioni 60 ili kutaka kumsajili kiungo wa Tottenham Eric Dier 23 (Mirror).

Manchester United hawatomuongeza mkataba Zlatan Ibrahimovic, 35, licha ya kumruhusu kuendelea kutumia uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Carrington wakati akiuguza jeraha lake la goti (Star).

Manchester United bado hawajaweza kutoa kiasi wanachotaka Inter Milan ili kumsajili winga Ivan Perisic, 28, lakini wanatazamia kukamilisha mkataba wa pauni kati ya milioni 45 hadi 50 (Independent).

Arsenal wana uhakika wa kutomuuza kiungo Alex Oxlade-Chamberlain, 23 ambaye amebakiza miezi 12 tu kwenye mkataba wake wa sasa (Daily Mail).

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger pia amedhamiria kutomuuza Alexis Sanchez, 28, ambaye hajasaini mkataba mpya na inadhaniwa anataka kwenda Manchester City (Independent).

Arsene Wenger hataki kumuuza Olivier Giroud, 30, mpaka suala la Alexis Sanchez na Thomas Lemar litakapotatuliwa (Daily Telegraph).

Arsenal watapambana na Liverpool katika kutaka kumsajili beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26 (Sun).

Chelsema wameweka kipaumbele katika kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, huku kukiwa hakuna uhakika na hatma ya Diego Costa, 28 (Guardian).

Diego Costa yuko tayari kuichezea Chelsea na kufikia muafaka na meneja wake Antonio Conte (Star).

Roma wanataka kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial, 21, lakini Old Trafford huenda wakapinga hatua hiyo (Mirror).

Manchester City wapo tayari kutoa pauni milioni 27 kumsajili beki wa kati wa Real Sociedad Inigo Martinez, 26 (Marca).

Meneja wa Leicester amekuwa na mazungumzo na winga Demarai Gray, 21, na anataka mchezaji huyo asiondoke huku Liverpool, Tottenham na Everton zikimtaka (Sky Sports).

Leicester City wamekubaliana kimsingi na Manchester City kuhusu kumsajili mshambuliaji Kelechi Iheanacho, 20 (Sky Sports).

James Rodriguez, 26, anataka hatma yake ifahamike mara moja, huku Real Madrid wakitaka pauni milioni 62. Manchester United na timu kadhaa Ulaya zimeambiwa zinaweza kupanda dau (Mail).

Tottenham watakuwa na mazungumzo na Estudiantes wiki hii kuhusiana na usajili wa beki Juan Foyth, 19 (London Evening Standard).

Deportivo La Coruna hawana uhakika kama wataweza kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Lucas Perez, 28, msimu huu (FourFourTwo).

Burnley wanafikiria kumsajili kiungo wa Swansea Jack Cork, 28, lakini wamesema hawamtaki kiungo wa Stoke Glenn Whelan, 33 (Lancashire Telegraph).

Newcastle wanafikiria kumchukua kipa wa Paris Saint-Germain Alphonce Areola, 24 (France Football).

Newcastle watamkosa winga wa Manchester City Jesus Navas, 31, ambaye anakaribia kurejea Sevilla (Marca).

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez ametaka klabu yake kuongeza dau katika kumsajili winga wa Norwich Jacob Murphy (Daily Telegraph).

Paris Saint-Germain wanasubiri kuona kama wamefanikiwa kumshawishi Dani Alves, 34, asiende Manchester City (Daily Mail).

Brighton wanataka kumsajili kiungo wa Chelsea Izzy Brown, 20 (Brighton & Hove Independent).

Chelsea wanajiandaa kutoa pauni milioni 70 kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24 (AS).

Inter Milan watapambana na Manchester United kutaka kumsajili kiungo wa Chelsea Nemanja Matic, 28 (Corriere dello Sport).

Tottenham nao wanamtaka mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 20 (The Sun).

Newcastle wamemuulizia winga wa Middlesbrough Adama Troure, 21 (Chronicle).

Everton wanafikiria kumchukua mshambuliaji wa Crystal Palace Christian Benteke kuziba nafasi ya Romelu Lukaku. Everton pia wanamtaka Olivier Giroud au Edin Dzeko (Daily Mail).

Manchester United walikataa nafasi ya kumsajili Alexandre Lacazette na badala yake wakaamua kumfuatilia Romelu Lukaku (The Guardian).

Dani Alves bado hajaamua aende wapi huku Manchester City, Chelsea na Tottenham zikimtaka (Globo Esporte)

Atletico Madrid wamekubaliana mkataba wa euro milioni 45 na Monaco wa kumsajili Fabinho ambaye amehusishwa na Manchester United, PSG na Manchester City, lakini huenda akajiunga na Atletico baada ya adhabu yao kumalizika (AS).

Liverpool bado wanavutana na mshambuliaji wa Atletico Madrid Angel Correa ambaye ada yake ya uhamisho ya pauni milioni 25 imekubaliwa lakini mchezaji huyu anataka mshahara mkubwa kuliko Liverpool wanaotaka kutoa (Foot Mercato).

Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, baada ya kumkosa Romelu Lukaku na wapo tayari kulipa euro milioni 70 (Marca).

Marseille wanamtaka mshambuliaji wa Manchester City Wilfried Bony (The Sun).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Tafadhali share tetesi hizi na wapenda soka wote. Uwe na siku njema.

Monday, July 10, 2017

Usajili

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 10.07.2017
Everton wametoa dau jipya la pauni milioni 32 kumtaka kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27. Wakifanikiwa watakuwa wametuia zaidi ya pauni milioni 100 za usajili msimu huu (Daily Mail).

Baada ya kumsajili Romelu Lukaku, 24, kutoka Everton, Manchester United huenda wakamsajili kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko, 22, baada ya kukubaliana mkataba wa pauni milioni 35. Chelsea wanamtaka pia Bakayoko (Daily Star).

Arsenal wapo tayari kupanda dau la tatu la zaidi ya pauni milioni 45 kumtaka winga wa Monaco, Thomas Lemar, baada ya dau la pauni milioni 30 na 40 kukataliwa (Daily Mirror).

Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott, 28, amedhamiria kupigania nafasi yake Emirates, licha ya kuhusishwa na kuhamia West Ham kwa pauni milioni 20 (Daily Star)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anataka kuimarisha eneo la kiungo kwa kumsajili Marcelo Brozovic kutoka Inter Milan (ESPN).

Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny, 27,  ambaye amehusishwa na kuhamia Juventus, ameachwa kwenye kikosi kilichosafiri kwenda Australia kwa ajili ya mechi za kujiandaa na msimu mpya (Sun).

Chelsea wapo tayari kutoa euro milioni 80 kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata baada ya kumkosa Romelu Lukaku (AS).

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka kumsajili beki wa Estudiantes, Juan Foyth, 19 kwa pauni milioni 10 (Daily Mirror).

Real Madrid wapo tayari kumuuza kiungo Mateo Kovacic, na Tottenham wamehusishwa na kumchukua mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia (Evening Standard).

Cristiano Ronaldo atabakia Real Madrid msimu wa 2017-18 na hivyo kufuta uvumi wa kuhamia Manchester United (AS).

Newcastle wanajaribu kukamilisha usajili wa kiungo wa Norwich Jacob Murphy, 22, kwa pauni milioni 8.5, huku Southampton na Crystal Palace wakimtaka pia mchezaji huyo (Daily Mirror).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na wiki njema.

Saturday, July 8, 2017

Usajili

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 08.07.2017
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, yuko tayari kuwa na mazungumzo na Antonio Conte, na huenda akaichezea tena klabu hiyo msimu ujao. Costa alitumiwa ujumbe mfupi wa simu (SMS) na Conte kuambiwa kuwa hahitajiki tena Stamford Bridge (Sun).

Chelsea wanataka zaidi ya pauni milioni 60 kumuuza Diego Costa, na watamuuza hata ikiwa Romelu Lukaku ataamua kujiunga na Manchester United (Daily Mail).

Huku Romelu Lukaku akikaribia kujiunga na Manchester United, Chelsea sasa huenda wakaelekeza nguvu zao kumtaka Andrea Belotti, 23, kutoka Torino na watalazimika kulipa takriban pauni milioni 90 (Daily Mirror).

Mkataba wa Romelu Lukaku kutoka Everton kwenda Manchester United ni pauni milioni 75 za awali na ada hiyo itapanda hadi pauni milioni 90 (Sky)

Antonio Conte sasa anataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Man Utd Javier “Chicharito” Hernandez kwa pauni milioni 13.5 baada ya dau lao la dakika za mwisho kutaka kumsajili Lukaku kushindikana (The Sun).

Wayne  Rooney anajiandaa kukata mshahara wake kwa nusu hadi pauni 150,000 kwa wiki kujiunga na Everton kutoka Manchester United (Daily Mail).
Wayne Rooney amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili kwenda Everton kutoka Manchester United (Daily Star).

Manchester United wataelekeza nguvu zao kumtaka kiungo wa Tottenham Eric Dier, 23, kwa pauni milioni 50 mara watakapokamilisha mkataba wa Lukaku (Telegraph).

Manchester United wameongeza bidii katika mazungumzo ya kutaka kumsajili kiungo wa Real Madrid James Rodriguez (The Independent).

Manchester United watalazimika kusubiri hadi mwezi Januari kupanda dau kumtaka beki wa kulia wa Benfica Nelson Semedo (Correio da Manha).

Arsenal wanasubiri jibu kutoka Monaco kuhusu kupanda dau la pauni milioni 40 kumtaka winga Thomas Lemar, 21 (Football London).

Arsenal wanamtaka kipa wa Toulouse Alban Lafont, 18, ili kuwa mrithi wa Petr Cech, pia wanamfuatilia kipa Stephane Ruffier wa St Etienne (Le 10).

Meneja wa Leicester City Craig Shakespeare amemuambia winga Riyad Mahrez , 26 anayehusishwa na kuhamia Arsenal kuwa hatocheza ikiwa haoneshi kujituma (Daily Telegraph).

Arsenal hawatomuuza Alexis Sanchez, 28, au Alex Oxlade-Chamberlain, 23, kwa timu yoyote ya EPL, licha ya kuwa wachezaji hao wanakaribia mwisho wa mikataba yao (Daily Star).

Alexis Sanchez ameiambia Arsenal kuwa anataka kuondoka na kwenda Manchester City. Makubaliano yamefikiwa kati ya Sanchez na City kwa pauni milioni 46.5, lakini Arsenal wanasita kumuuza kwa timu hasimu ya EPL, lakini huenda akaondoka bure mwisho wa msimu ujao (El Mercurio).

Crystal Palace wanataka kupanda dau kumtaka kipa wa Barcelona Jasper Cillesen, 28, (AS).

Paris Saint-Germain wanaongoza mbio za kumsajili Gareth Bale kutoka Real Madrid (Don Balon).

West Ham wamepunguza kasi ya kutaka kumsajili kipa wa Man City Joe Hart na sasa wanatafuta mshambuliaji (Sun).

Liverpool wanasema timu kadhaa zimemuulizia beki wake Mamadou Sakho, na wana uhakika kuna timu itaweza kulipa pauni milioni 30 (Liverpool Echo).

Mshambuliaji wa Man City Wilfried Bony anavutia timu kadhaa za China na City wana imani watapata pauni milioni 14 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast (Independent).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema.

Friday, July 7, 2017

Usajili

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 07.07.2017
Mustakbali wa meneja wa Chelsea, Antonio Conte uko mashakani baada ya meneja huyo kukasirishwa na shughuli nzima ya usajili katika klabu hiyo (Daily Mirror).

Hatua ya Manchester United kutaka kumsajili Romelu Lukaku, 24, haihusiani na mkataba ambao utamrejesha Wayne Rooney, 31, Everton (Liverpool Echo).

Chelsea bado wanatarajiwa kujaribu  kumsajili Romelu Lukaku, 24, licha ya taarifa kuwa mchezaji huyo amekubali kuhamia Manchester United kwa pauni milioni 75 kutoka Everton (Guardian).

Mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, ameachwa “kwenye mataa” baada ya Manchester United kumsajili Romelu Lukaku. Morata alikuwa na uhakika kuwa anahamia Old Trafford (Independent).

Romelu Lukaku amekubali kusaini mkataba wa muda mrefu Manchester United na mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki (Daily Star).

Chelsea huenda wakakabiliwa na tatizo la mshambuliaji baada ya Diego Costa kuanza kuaga wachezaji wenzake kufuatia kuambiwa na Antonio Conte kuwa hayuko kwenye mipango yake msimu ujao (Daily Telegraph).

Chelsea wanajiandaa kutoa dau “kubwa” kumtaka kiungo wa Real Madrid James Rodriguez (AS).

Chelsea sasa wameelekeza macho yao kwa mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente, 32, baada ya kushindwa kumpata kwa mkopo mwezi Januari (Evening Standard).

Barcelona wamekasirishwa na nahodha wao wa zamani Carles Puyol, baada ya mchezaji anayemwakilisha Eric Garcia, 16, kuamua kuhamia Manchester City (Independent).

Everton wanajiandaa kupanda dau jipya la pauni milioni 32 kumtaka kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27 (Daily Mail).

Kipa wa Stoke City Jack Butland, 24, amesema anaweza ‘kufikiria’ iwapo Manchester United watamtaka (Manchester Evening News).

Arsenal wanamtaka kiungo wa Eintracht Frankfurt Aymen Barkok, 19 (Spox).

Marseille wanaongoza katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30, kwa kitita cha pauni milioni 24.7, baada ya Arsenal kufanikisha usajili wa Alexandre Lacazette (Daily Telegraph).

Arsenal hawataki kulipa kiasi ambacho Leicester wanakitaka ili kumsajili winga Riyad Mahrez, 26, ambaye anatarajiwa kuondoka Leicester msimu huu (Daily Star).

Barcelona wapo tayari kutoa pauni milioni 26 kumsajili beki wa Arsenal Hector Bellerin (Sport).

Arsenal wanamfuatilia kiungo wa Monaco Fabinho (France Football).

Winga wa zamani wa Newcastle Hatem Ben Arfa, 30, ameambiwa anaweza kuondoka Paris Saint-Germain (L’Equipe).

Paris Saint-Germain watamgeukia Philippe Coutinho iwapo watashindwa kumsajili Kylian Mbappe kutoka Monaco. PSG wapo tayari kutoa pauni milioni 70 kumchukua Coutinho (Le10sport).

Winga Demarai Gray, 21, anataka kuhakikishiwa namba Leicester huku Tottenham na Liverpool zikimnyatia (Daily Mirror).

Dau la pauni milioni 22 la Barcelona kumtaka kiungo wa zamani wa Tottenham, Paulinho, 28, limekataliwa na klabu yake ya Guangzhou Evergrande (Sky Sports).

Licha ya Guangzhou Evergrane kukataa, Barcelona watarejea na dau jingine kumtaka Paulinho (Cadena SER).

Stoke City wamekuwa na mazungumzo na Manchester City ya kumsajili kiungo Fabien Delph, 27 (Stoke Sentinel).

Real Madrid wamekuwa na mazungumzo ya siri na PSG kuhusu Marco Verratti,24 (Don Balon).

Real Madrid wamekuwa na mazungumzo mapya na Kylian Mbappe (Marca).

Real Madrid watakuwa tayari kumruhusu Gareth Bale kuondoka kwa pauni milioni 88 (Diario Gol).

Watford wanazungumza na Chelsea kuhusu kiungo Nathaniel Chalobah, 22, na wana uhakika mchezaji huyo anataka kurejea Vicarage Road (London Evening Standard).

Aston Villa wamemuulizia kipa wa Manchester City Joe Hart (Birmingham Mail).

AC Milan sasa wamemgeukia mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, na pia wanamtaka Nikola Kalinic (Gianluca Di Marzio).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema.

Thursday, July 6, 2017

Usajili

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 06.07.2017
Manchester United wanakaribia kuwapiku Chelsea na kumsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, 24,  kwa kutoa kitita kitakachovunja rekodi ya dunia cha pauni milioni 100 (Daily Mail).

Manchester United wametoa dau la pauni milioni 66 kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, na huenda makubaliano kati ya timu hizo mbili yakafikiwa katika saa chache zijazo (Marca).

Manchester United wangependa kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund Julian Weigl baada ya kushindwa kuwapata Eric Dier kutoka Tottenham na Nemanja Matic kutoka Chelsea (Daily Mail).

Paris St-Germain wapo tayari kutoa pauni milioni 70 kutaka kumsajili kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25 (Le10 Sport).

Atletico Madrid wanajiandaa kutoa dau rasmi la pauni  milioni 22 kutaka kumsajili Diego Costa, 28, kutoka Chelsea (Guardian).

Hatua ya Atletico Madrid kutaka kumsajili tena Diego Costa itategemea kama wataruhusiwa kumpeleka China kwa mkopo hadi adhabu yao ya usajili itakapomalizika mwezi Januari (Mirror).

Chelsea wamefikia makubaliano na Roma ya kumsajili beki Antonio Rudiger, 24 kwa pauni milioni 34, ingawa mchezaji huyo bado hajafikia makubaliano rasmi kuhusu maslahi binafsi (Sky Sports).
Meneja wa zamani wa Liverpool Gerard Houllier anasema Arsenal huenda wamempata ‘Ian Wright mpya’ baada ya kumsajili Alexandre Lacazette (TalkSport).

Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, anataka mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki, ambao ni ongezeko la pauni 125,000 kwa wiki katika mshahara wake wa sasa (Daily Mirror).

Arsenal wametoa dau jipya kwa Monaco kutaka kumsajili winga Thomas Lemar (Evening Standard).

West Ham wanaonekana kuongoza katika mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Burnley Andre Gray, 26, kwa pauni milioni 15 (Evening Standard).

Huddersfiled waliopanda daraja EPL wanakaribia kumsajili beki Mathias Jorgensen, 27, kutoka FC Copenhagen kwa pauni milioni 3.5 (Sun).

Kiungo wa Chelsea Nathaniel Chalobah, 22, anazungumza na Watford kutaka kuhamia katika timu hiyo aliyoichezea kwa mkopo msimu wa 2012-13 (Daily Mirror).

Dau la pauni milioni 3 la Burnley la kumtaka mshambuliaji wa Stoke City Jonathan Walters limekubaliwa (Sky Sports).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Tafadhali share tetesi hizi na wapenda soka. Uwe na siku njema.

Usajili

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 06.07.2017
Manchester United wanakaribia kuwapiku Chelsea na kumsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, 24,  kwa kutoa kitita kitakachovunja rekodi ya dunia cha pauni milioni 100 (Daily Mail).

Manchester United wametoa dau la pauni milioni 66 kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, na huenda makubaliano kati ya timu hizo mbili yakafikiwa katika saa chache zijazo (Marca).

Manchester United wangependa kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund Julian Weigl baada ya kushindwa kuwapata Eric Dier kutoka Tottenham na Nemanja Matic kutoka Chelsea (Daily Mail).

Paris St-Germain wapo tayari kutoa pauni milioni 70 kutaka kumsajili kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25 (Le10 Sport).

Atletico Madrid wanajiandaa kutoa dau rasmi la pauni  milioni 22 kutaka kumsajili Diego Costa, 28, kutoka Chelsea (Guardian).

Hatua ya Atletico Madrid kutaka kumsajili tena Diego Costa itategemea kama wataruhusiwa kumpeleka China kwa mkopo hadi adhabu yao ya usajili itakapomalizika mwezi Januari (Mirror).

Chelsea wamefikia makubaliano na Roma ya kumsajili beki Antonio Rudiger, 24 kwa pauni milioni 34, ingawa mchezaji huyo bado hajafikia makubaliano rasmi kuhusu maslahi binafsi (Sky Sports).
Meneja wa zamani wa Liverpool Gerard Houllier anasema Arsenal huenda wamempata ‘Ian Wright mpya’ baada ya kumsajili Alexandre Lacazette (TalkSport).

Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, anataka mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki, ambao ni ongezeko la pauni 125,000 kwa wiki katika mshahara wake wa sasa (Daily Mirror).

Arsenal wametoa dau jipya kwa Monaco kutaka kumsajili winga Thomas Lemar (Evening Standard).

West Ham wanaonekana kuongoza katika mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Burnley Andre Gray, 26, kwa pauni milioni 15 (Evening Standard).

Huddersfiled waliopanda daraja EPL wanakaribia kumsajili beki Mathias Jorgensen, 27, kutoka FC Copenhagen kwa pauni milioni 3.5 (Sun).

Kiungo wa Chelsea Nathaniel Chalobah, 22, anazungumza na Watford kutaka kuhamia katika timu hiyo aliyoichezea kwa mkopo msimu wa 2012-13 (Daily Mirror).

Dau la pauni milioni 3 la Burnley la kumtaka mshambuliaji wa Stoke City Jonathan Walters limekubaliwa (Sky Sports).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Tafadhali share tetesi hizi na wapenda soka. Uwe na siku njema.

Wednesday, July 5, 2017

Usajili

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO 05.07.2017
Alexandre Lacazette amekamilisha vipimo vya afya Emirates na mkataba wake wa miaka mitano wa pauni milioni 52 unatazamiwa kuthibitishwa baadaye leo (BBC, Sky).

Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney, 31, ameondolewa kwenye kikosi kitakachosafiri kwenda Marekani, na atakamilisha uhamisho wake wa bila malipo kurejea Everton mwishoni mwa wiki. Everton pia wanataka kumsajili Olivier Giroud, 20, kutoka Arsenal kwa pauni milioni 20 (Sun).

Manchester United wanataka kupanda dau jipya kumtaka winga wa Inter Milan Ivan Perisic, 28 (Sky Italia).

Manchester United watafanya jaribio la mwisho kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, wiki hii, huku Real wakigoma kushusha bei ya pauni milioni 72 (Independent).

Beki wa Roma Antonio Rudiger, 24, amewasili London kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 36 kwenda Chelsea (Daily Mirror).

Chelsea wanafikiria kumchukua pia kipa wa Paris Saint-Germain Alphonse Areola, 24 (Transfermarketweb).

Manchester City wamekataa ombi la Newcastle United kumchukua kipa Joe Hart, 30, kwa mkopo (Daily Mail).

Mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 18, ametoa sharti la kuwa mchezaji anayelipwa zaidi- nyuma tu ya Cristiano Ronaldo- iwapo Real Madrid wanataka kumsajili (Diario Gol).

Meneja wa Leicester City ametoa dau la pauni milioni 20 kumtaka mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 29 (Daily Mirror).

Tottenham wanataka kumchukua kiungo wa Everton Ross Barkley, 23, lakini hawapo tayari kulipa pauni milioni 50 wanazotaka Everton (Sun).

Liverpool wametoa dau la pauni milioni 14.9 kutaka kumsajili beki wa Lyon Emanuel Mammana, 21 (Sport Review).

Juventus wamempa beki wao Alex Sandro, 26, mshahara wa pauni 84,000 kwa wiki ili kumshawishi asiondoke kwenda Chelsea ambao wapo tayari kutoa pauni milioni 61 kumnunua (London Evening Standard).

Kiungo wa Arsenal Santi Carzola, 32, ambaye hajacheza tangu Oktoba 2016, huenda akakosa msimu ujao wote wa 2017/18 kutokana na kuwa majeruhi bado (Daily Express).

Beki wa Arsenal Hector Bellerin, 22, ameiambia klabu yake kuwa anataka kuondoka, lakini meneja Arsene Wenger amekataa ombi lake la kutaka kuondoka. Barcelona wanataka kumsajili beki huyo kwa pauni milioni 35 (Daily Express).

Tottenham wanataka kumsajili Alfie Mawson, 23, kutoka Swansea, au Ben Gibson, 24, kutoka Middlesbrough, huku wakitaka kumuuza beki wao wa kati Kevin Wimmer, 24 kwa pauni milioni 20 (Daily Mirror).

Dau la pauni milioni 8 kumsajili mshambuliaji Britt Assombalonga, 24, limekataliwa na Nottingham Forest (Daily Mail).

Crystal Palace wanafikiria kusajili mabeki wawili Joel Veltman, 25, na Kenny Tete, 21, kutoka Ajax kwa pauni milioni 10 (Guardian)

Newcastle wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Burnley Andre Gray, 26 (Shie;ds Gazette).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema.

Saturday, July 1, 2017

Usajili

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 01.07.2017
*Dirisha la usajili limefunguliwa rasmi

Arsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette, 26. Usajili wa Lacazette unatarajiwa kuvunja rekodi ya Arsenal ya pauni milioni 42.4 walizotoa kumsajili Mesut Ozil kutoka Real Madrid mwaka 2013 (BBC Sport).

Chelsea wanapanga kutumia pauni milioni 125 kusajili wachezaji watatu. Kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko, 22, Antonio Rudiger, 24, kutoka Roma na beki wa kushoto wa Juventus Alex Sandro, 26 ambaye huenda akagharimu pauni milioni 60 (Daily Telegraph).

Chelsea wanafikiria kumsajili beki wa kushoto wa Porto Alex Telles, 24, iki watamkosa Sandro ambaye pia ananyatiwa na Paris St-Germain (Sun).

Mshambuliaji wa Real Madfrid Alvaro Morata, 24, amewaambia marafiki wake kuwa ameamua kujiunga na Manchester United na kuwa mkataba kati ya OT na Real Madrid umekamilika (Daily Express).

Meneja wa zamani wa Spain na Real Madrid Vincente del Bosque ameiomba Real Madrid kutomuuza Alvaro Morata (Daily Express).

Manchester United watajaribu kumsajili kipa wa Manchester City Joe Hart, 30, iwapo David de Gea, 26, atakwenda Real Madrid (Sun).

Manchester United bado hawajafanikiwa kumpata Ivan Perisic, 28, na mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia amemwambia wakala wake kulazimisha uhamisho wake kwenda Uingereza (Goal).

West ham wameshindwa kuwapata Anthony Modeste, 29, kutoka FC Cologne na Cedric Bukambu, 25, kutoka Sevilla, kwa sababu dau lao la pauni milioni 22, kwa kila mchezaji limekataliwa (Daily Telegraph).

Kiungo wa Chelsea Nathaniel Chalobah, 22, anasita kusaini mkataba mpya mpaka atakapohakikishiwa kuwa atapata namba katika kikosi cha kwanza Stamford Bridge (Independent).

Watford wanafikiria kumchukua Nathaniel Chalobah, ambaye ameonesha kiwango cha juu katika michuano ya chini ya umri wa miaka 21 iliyomalizika nchini Poland (Sky Sports).

Southampton wanakaribia kufanya usajili wao wa kwanza kwa kumchukua beki Jan Bednarek, 21, kutoka Lech Poznan ya Poland (Daily Echo).

Mchambuzi wa soka Ulaya Gabriele Marcotti anaamini Liverpool tayari wamekubaliana maslahi binafsi na kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 (Bleacher Report).

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameweka  kipaumbele kumsajili Nemanja Matic, 28, huku mchezaji aliyekuwa akimtaka- Fabinho, 23, wa Monbaco akielekea Paris St-Germain (Manchester Evening News).

Jose Mourinho anataka kumsajili beki wa Celtic Kieran Tierney, 20, kwa pauni milioni 20 (Daily Mirror).

Jose Mourinho amekasirishwa na kasi ndogo ya Manchester United ya usajili, kwa kuwa mpaka sasa wamesajili mchezaji mmoja tu mwenye ‘jina’ (The Sun).

Beki wa kushoto wa Leeds United Charlie Taylor, 23, anajiandaa kujiunga na Burnley, baada ya kuwepo Leeds kwa miaka 14 (Yorkshire Evening Post).

Meneja mpya wa Middlesbrough Garry Monk yuko tayari kuwazidi kete Leeds United kwa kumsajili kiungo wa Norwich Jonny Howson, 29 (Daily Mirror).

Kiungo wa zamani wa Newcastle, Mehdi Abeid, 24, amesema itakuwa heshima kubwa kurejea tena St James Park. Kiungo huyo aliondoka Newcastle miaka miwili iliyopita na kwenda Panathinaikos na Dijon (Newcastle Chronicle).

West Brom wamekubaliana ada ya uhamisho ya pauni milioni 12 na Southampton ya kumsajili mshambuliaji Jay Rodriguez, 27 (Telegraph).

West Ham wanataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez, 29, ambaye alijiunga na Bayer Leverkusen mwaka 2015 (Bild).

Borussia Dortmund wametangaza kusajili wachezaji wanne Maximilian Philipp, Dan-Axel Zagadou, Omer Toprak na Mahmoud Dahoud.

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa.  Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Siku njema.