Friday, April 8, 2016

Maasi ya kikurd 1991

wenzako Mpiga picha Richard Wayman anakumbuka akifanya kazi maeneo ya kaskazini mwa Iraq wakati wa maasi ya Wakurdi mwaka 1991. Baada ya zaidi ya mwezi wa mashambulio ya angani na kipindi kifupi cha mashambulio ya ardhi ya wanajeshi wa muungano ulioongozwa na Marekani dhidi ya wanajeshi wa Saddam Hussein, Vita vya Ghuba vya 1991 vilikaribia kumalizika. Lengo la kukomboa Kuwait iliyokuwa imevamiwa na kutekwa mwaka uliotangulia lilitimizwa lakini Saddam alisalia mamlakani na aliwageukia Wakurdi na makundi ya Kishia. Mpiga picha Richard Wayman alikuwa amefanya kazi na makundi mengi ya Wakurdi Iraq na Uturuki miaka ya 1980 na aliamua alihitaji kuwa huko. Anakumbuka akifuatilia vita hivyo vya uasi 1991. "Nilikuwa mpiga picha wa kujitegemea na kutoka London nilijaribu kufanya mipango ya kufika maeneo ya Wakurdi Iraq haraka." "Jeshi la Uturuki lilikuwa limefunga mpaka na wanahabari walisubiri katika mji wa mpakani wa Cizre kuruhusiwa kuvuka. Baada ya siku nyingi za kujaribu kupita kisheria bila mafanikio, niliungana na wachumba kutoka kituo cha televisheni cha ZDF TV ya Ujerumani na tukaelekea Silopi - karibu zaidi na mpaka. Baada ya kufanya urafiki na walinzi wa Uturuki tulifanikiwa kuvuka mpaka katika Mto Khabur." "Usiku mmoja kukiwa na giza, tulisukuma mtumbwi wetu mtoni na kuvuka. Upande ule mwingine, tulikutana na kundi la wapiganaji wa Peshmerga wa Kikurdi ambao walitupeleka hadi ngome yao. Wakurdi walikuwa wana furaha, walikuwa wameuteka mji wenye mafuta mengi wa Kirkuk kutoka kwa wanajeshi wa Saddam. Lakini mambo yalianza kubadilika upesi, siku chache tu baadaye, wanajeshi wa serikali waliungana na kuanza kupigana kukomboa maeneo waliyopoteza. Walisaidiwa na hali kwamba nusu ya vifaru vya wanajeshi waaminifu kwa Saddam wa Republican Guard walikuwa wamefanikiwa kutoroka vita Kuwait" "Isitoshe, makubaliano ya kusitisha Vita vya Ghuba yalikuwa yamewazuia wanajeshi wa Iraq dhidi ya kutumia ndege za kawaida anga ya nchi hiyo na badala yake kuwataka watumie tu helikopta kwa sababu madaraja yalikuwa yameharibiwa. Mataifa ya muungano yalikuwa yamekubali ombi la Iraq kutumia helikopta ili kusafirisha maafisa wa serikali. Walizitumia kuzima maasi." Wapiganaji wa Kikurdi walijaribu kupunguza kasi ya wanajeshi wa Republican Guard kuwezesha raia kutoroka maeneo ya Wakurdi na kukimbilia Uturuki na Iran lakini walizidiwa nguvu upesi. Nilitoroka na wakimbizi hadi Uturuki baada ya kutembea siku mbili. Wakurdi waliogopa Saddam angetumia silaha za kemikali kama alivyofanya 1988. Ndoto nyingine ya Wakurdi kujipatia uhuru ilizimwa tena. Zaidi ya Wakurdi milioni moja walikimbilia katika mipaka ya Uturuki na Iran wakijaribu kutoroka. Wengi walifia milimani kabla ya majeshi ya muungano ulioongozwa na Marekani kutengeneza kambi na maeneo salama upande wa Iraq." Picha zote na Richard Wayman

No comments:

Post a Comment