Saturday, July 1, 2017

Usajili

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 01.07.2017
*Dirisha la usajili limefunguliwa rasmi

Arsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette, 26. Usajili wa Lacazette unatarajiwa kuvunja rekodi ya Arsenal ya pauni milioni 42.4 walizotoa kumsajili Mesut Ozil kutoka Real Madrid mwaka 2013 (BBC Sport).

Chelsea wanapanga kutumia pauni milioni 125 kusajili wachezaji watatu. Kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko, 22, Antonio Rudiger, 24, kutoka Roma na beki wa kushoto wa Juventus Alex Sandro, 26 ambaye huenda akagharimu pauni milioni 60 (Daily Telegraph).

Chelsea wanafikiria kumsajili beki wa kushoto wa Porto Alex Telles, 24, iki watamkosa Sandro ambaye pia ananyatiwa na Paris St-Germain (Sun).

Mshambuliaji wa Real Madfrid Alvaro Morata, 24, amewaambia marafiki wake kuwa ameamua kujiunga na Manchester United na kuwa mkataba kati ya OT na Real Madrid umekamilika (Daily Express).

Meneja wa zamani wa Spain na Real Madrid Vincente del Bosque ameiomba Real Madrid kutomuuza Alvaro Morata (Daily Express).

Manchester United watajaribu kumsajili kipa wa Manchester City Joe Hart, 30, iwapo David de Gea, 26, atakwenda Real Madrid (Sun).

Manchester United bado hawajafanikiwa kumpata Ivan Perisic, 28, na mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia amemwambia wakala wake kulazimisha uhamisho wake kwenda Uingereza (Goal).

West ham wameshindwa kuwapata Anthony Modeste, 29, kutoka FC Cologne na Cedric Bukambu, 25, kutoka Sevilla, kwa sababu dau lao la pauni milioni 22, kwa kila mchezaji limekataliwa (Daily Telegraph).

Kiungo wa Chelsea Nathaniel Chalobah, 22, anasita kusaini mkataba mpya mpaka atakapohakikishiwa kuwa atapata namba katika kikosi cha kwanza Stamford Bridge (Independent).

Watford wanafikiria kumchukua Nathaniel Chalobah, ambaye ameonesha kiwango cha juu katika michuano ya chini ya umri wa miaka 21 iliyomalizika nchini Poland (Sky Sports).

Southampton wanakaribia kufanya usajili wao wa kwanza kwa kumchukua beki Jan Bednarek, 21, kutoka Lech Poznan ya Poland (Daily Echo).

Mchambuzi wa soka Ulaya Gabriele Marcotti anaamini Liverpool tayari wamekubaliana maslahi binafsi na kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 (Bleacher Report).

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameweka  kipaumbele kumsajili Nemanja Matic, 28, huku mchezaji aliyekuwa akimtaka- Fabinho, 23, wa Monbaco akielekea Paris St-Germain (Manchester Evening News).

Jose Mourinho anataka kumsajili beki wa Celtic Kieran Tierney, 20, kwa pauni milioni 20 (Daily Mirror).

Jose Mourinho amekasirishwa na kasi ndogo ya Manchester United ya usajili, kwa kuwa mpaka sasa wamesajili mchezaji mmoja tu mwenye ‘jina’ (The Sun).

Beki wa kushoto wa Leeds United Charlie Taylor, 23, anajiandaa kujiunga na Burnley, baada ya kuwepo Leeds kwa miaka 14 (Yorkshire Evening Post).

Meneja mpya wa Middlesbrough Garry Monk yuko tayari kuwazidi kete Leeds United kwa kumsajili kiungo wa Norwich Jonny Howson, 29 (Daily Mirror).

Kiungo wa zamani wa Newcastle, Mehdi Abeid, 24, amesema itakuwa heshima kubwa kurejea tena St James Park. Kiungo huyo aliondoka Newcastle miaka miwili iliyopita na kwenda Panathinaikos na Dijon (Newcastle Chronicle).

West Brom wamekubaliana ada ya uhamisho ya pauni milioni 12 na Southampton ya kumsajili mshambuliaji Jay Rodriguez, 27 (Telegraph).

West Ham wanataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez, 29, ambaye alijiunga na Bayer Leverkusen mwaka 2015 (Bild).

Borussia Dortmund wametangaza kusajili wachezaji wanne Maximilian Philipp, Dan-Axel Zagadou, Omer Toprak na Mahmoud Dahoud.

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa.  Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Siku njema.

No comments:

Post a Comment