Friday, March 25, 2016

Wkb

Waholanzi walivyonaswa wakisafirisha Tumbili 61, uwanja wa ndege KIA. VYOMBO vya ulinzi na usalama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) vimefanikiwa kuwanasa wafanyabiashara wawili ndugu, raia wa Uholanzi wakiwa katika harakati ya kusafirisha wanyama Hai 61,aina ya Tumbili kuelekea nchini Armenia. Wanyama hao wakiwa kwenye makasha sita tofauti ya kuhifadhia wanyama walikuwa wasafirishwe kwa ndege maalumu ya mizigo yenye namba EW/364G iliyosajiliwa nchini Belarus kupitia kampuni ya Arusha Freight Limited ya jijini Arusha. Raia hao wa Uholanzi waliokamatwa juzi majira ya saa 1:30 jioni katika uwanja wa ndege wa KIA wametambulika majina yao kuwa ni Arten Vardanian (52) aliyekuwa na hati ya kusafiria yenye namba NWF8CKJR8 na Edward Vardanian (46) aliyekuwa na hati ya kusafiria namba NY969P96.

No comments:

Post a Comment